Mkuu wa Tawi la Utumishi Jeshini Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Fatma Mwasa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo tarehe 20 Februari 2025.
Amemuhakikishia kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania litaendelea kuhakikisha eneo lote la Mkoa wa Kagera linakuwa salama ili kuruhusu wananchi kufanya shughuli za maendeleo kwa uhuru.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Fatma Mwasa amelishukuru JWTZ kwa namna linavyohakikisha mpaka wa Tanzania kwa upande wa Mkoa wa Kagera liko salama wakati wote.
Amemuhakikishia Meja Jenerali Gaguti kuwa uongozi wa Mkoa utaendelea kutoa ushirikiano kwa JWTZ katika mambo yote ambayo utahusishwa.
Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti na ujumbe wake yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.