Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishuhudia makabidhiano ya matrekta kati ya Wizara ya Kilimo na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Februari 22, 2025. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Frank Chonya na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mohamed Omary. Wilaya ya Ruangwa imepokea Matrekta matano ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kukabidhi zana za kilimo kwenye vituo 45 vya kutolea huduma nchini. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishuhudia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Frank Chonya akiwa ndani ya moja ya matreka matano yaliyokabidhiwa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kituo cha kutolea huduma ya zana za kilimo, kilichopo Wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yamefanyia Februari 22, 2025. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mhe. Hassan Jarufu na Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ruangwa Ibrahim Ndoro (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Ruangwa, wakati wa Halfa ya kushuhudia awamu ya kwanza ya makabidhiano matreka matano kwa ajili ya kituo cha kutolea huduma za zana za kilimo, ikiwa ni mapngo wa Serikali wa kukabidhi zana za kilimo kwenye vituo 45 vya kutolea huduma nchini, Februari 22, 2025. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)