Na Prisca Libaga , Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Leo Jumamosi Machi 01, 2025 amekuwa miongoni mwa waliojitokeza kushuhudia mechi ya ligi kuu Tanzania bara, kati ya Coastal Union na Simba, Mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha na kushuhudia Simba Sc ikiibuka na ushindi wa magoli 3-0, magoli yaliyofungwa na mchezaji Steven Desse Mukwala.





