Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungunza na waandishi wa habari wakati akitangaza maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya VET Profesa Sifuni Mchome akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore wakimsukiliza Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda hayupo pichani wakati akitangaza maadhimisho ya Miaka 30 ya VETA jijini Dar es Salaam.
*Profesa Mkenda atangaza maadhimisho ya miaka 30 ya VETA na mafanikio yake
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema kuwa Mamlaka ya Elimu Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) itengeneze mpango kazi katika kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwezesha vijana wenye mafunzo ya ufundi stadi wanakuwa uwanja mpana kujiajiri na kuleta maendeleo nchini.
Hayo ameyasema Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akitangaza maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambayo yatakayoanza Machi 8 hadi 21 kwa kuhitimishwa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa.
Amesema kuwa kuna mafundi ambao hawana hawajapita katika vyuo vya VETA lakini ni wabunifu ambao nao washirikishwe kupata mafunzo na kutoa ujuzi huo kwa wanafunzi waliopo na baadae kuungana katika uzalishaji na bidhaa pamoja na ufundi kwenye sekta mbalimbali.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Ukuzaji Stadi na Ubunifu kwa Maendeleo ya Jamii na Taifa’.
Waziri Mkenda amesema shughuli mbalimbali zitafanyika katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho hayo, ikiwemo kutoa huduma kwa jamii, kuendesha maonesho ya teknolojia na ujuzi, pamoja na kutoa tuzo na vyeti vya heshima kwa watu mbambali kwa mchango wao katika shughuli za maendeleo ya Ufundi Stadi nchini.
Amesema mwaka huu wataadhimisha miaka 30 ya VETA ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge mwaka 1994 na kuanza kazi rasmi mwaka 1995. Kabla ya VETA kulikuwa na Idara ya Mafunzo na Majaribio ya Ufundi Stadi (NVTD) katika Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii ambayo ilianzishwa mwaka 1975.
Amesema kwa kipindi cha miongo mitatu ya VETA imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwajengea Watanzania uwezo wa kujiajiri, kuajiriwa, na kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi.
Aidha amesema kuwa VETA imekuwa na mafanikio na kuwa taasisi muhimu inayochangia rasilimali watu yenye ujuzi inayohudumu katika sekta mbalimbali, ikiwemo Viwanda, Kilimo, Ujenzi, Teknolojia, Nishati na huduma na Utalii.
Amesema kuwa, maadhimisho hayo pia ni fursa ya kipekee kwa jamii kusherehekea mchango wa ufundi stadi katika maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii, huku tukijipanga kuimarisha sekta ya ufundi stadi ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na mahitaji ya soko la ajira.
“Maadhimisho haya ya miaka 50 ya utoaji elimu na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na miaka 30 ya VETA yanakuja wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza kukamilishwa ujenzi wa vyuo vya VETA vya hadhi ya kimkoa, katika mikoa yote ambayo haina vyuo vya VETA na vyuo vya VETA vyenye hadhi ya kiwilaya katika wilaya zote ambazo hazina vyuo hivyo.
Amesema sasa VETA inakamilisha ujenzi wa chuo chenye hadhi ya Mkoa cha VETA kwa Mkoa wa Songwe na tunaendelea na ujenzi wa vyuo 64 katika wilaya 64 ambazo zilikuwa hazina vyuo hivyo.
“Nitumie fursa hii kuwakaribisha wadau wote katika maadhimisho haya yanayoendelea nchini na upekee katika kilele cha yatayofanyika jijini Dar es Salaam ili tujionee na kujadili umuhimu wa elimu na ujuzi kulingana na mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo yam waka 2014 toleo la 2023,” amesema Profesa Mkenda