Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marie stopes, Patrick Kinemo akizungumza kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika hafla iliyoandaliwa na Maria stopes na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa Afya kutoka serikalini, Bima za Afya na mashirika mbali mbali yanayotekeleza masuala ya Afya ua uzazi.
Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha mama na mtoto na bijana wizara ya Afya, Felix Bundala akizungumza kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika hafla iliyoandaliwa na Maria stopes na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa Afya kutoka serikalini, Bima za Afya na mashirika mbali mbali yanayotekeleza masuala ya Afya ua uzazi.

SHIRIKA la Marie Stopes Tanzania (MST) limesema katika kipindi cha mwaka 2024 kupitia huduma za Mkoba imefanikiwa kufikia takribani wateja milioni 2 kati ya hao asilimia 20 walikuwa vijana ukilinganisha na mwaka 2023/24 sawa na ongezeko la asilimia 21.
Takwimu hizo zimetolewa Machi 5,2025 na Mkurungenzi Mkaazi wa Marie Stopes Tanzania, Patrick Kinemo kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8, kila mwaka.
“Kati ya hao milioni 2 wanaume walikuwa ni asilimia 4 tu hivyo ni wazi ushiriki wao ni kidogo na wanahitaji kuhamasishwa ilikuongeza uelewa juu ya afya ya uzazi pia wakitumia impact calculator utakuta kwenye wateja hao waliofikiwa watakuwa wamekinga mimba zisizotarajiwa zaidi ya milioni 2 kwa kipindi cha miaka mitano na kuzuia vifo 3430 kwa kipindi hicho,”Amesema Kinemo
Amesema Shirika hilo limekuwa likifanya kazi kwa kushirikiana na serikali kwa kuwajengea uwezo wa hudumu wa afya katika vituo 343 pamoja na manesi wao 43 kusaidia wanaosaidia kutoa huduma.
Amesema kwa hapa Tanzania wanakliniki tisa ikiwemo ya martenity iliyopo Mwenge pamoja na dawa za afya ya uzazi ambazo utolewa kama huduma ambazo zilizowekezwa kwa mwanamke kwani anapotumia uzazi wa mpango inamsaidia kutunza na kupanga watoto anao wahitaji.
“Familia inapanga ni lini apate mtoto mwingine na faida kubwa afya ya mama inakuwa nzuri na mtoto akaimalika kwani Kuna kuwa na hatua kati ya mtoto mmoja na mwingine,hivyo kwa miaka mitano tutaweza kuepusha vifo,”amesema Kinemo
Ameongeza,”Nchi inajipanga ilikuendelea kuhakikisha huduma zinatolewa hata kama USAID akiwa hayupo kwa kuhakikisha wale wanaoweza kuchangia huduma hiyo mashiriki kwa kutumia sekta binafsi pamoja na huduma ya bima kwa kufanya hivyo mwanamke atasaidia kukuza Uchumi wa nchi na kupunguza utegemezi kwani ataweza kushiriki katika uzalishaji,”
Kinemo amesema suala la mila potofu bado ni changamoto kubwa kwani inakwamisha kufikia watu wengi zaidi,hivyo elimu iendelee kutolewa hasa mikoa ya Kanda ya ziwa hivyo ni lazima jamii iwe na taarifa sahihi juu ya namna ya kujikinga.
Mkurungenzi Msaidizi Wizara ya Afya anayesimamia huduma za afya ya mtoto na Vijana,Idara ya Afya na Uzazi, Mama na Mtoto, Dkt. Felix Bundala amesema serikali inajivunia kushirikiana na mashirika kama Marie Stopes kwani inasaidia kupunguza vifo na changamoto za uzazi.
“Huduma hizi zinahusisha kinga pamoja na matibabu kwa makundi ya vijana na watu wazima hivyo jamii lazima iwe na taarifa sahihi za namna ya kujingika na kutoa taarifa ili kujikinga na mimba za mapema na utotoni kwani mimba hizo zimekuwa zikisababisha vifo vya uzazi pamoja na kujikinga na Magonjwa kama UKIMWI,”amesema dk Bundala.
Amesema ni muhimu elimu ya uzazi ikatolewa iliwazazi waweze kujua ni lini wanatakiwa kupata mtoto au nafasi kati ya mtoto mmoja na mwingine ni wakati gani lengo ni kulinda afya ya mama,mtoto na baba.
Bundala anasema kupitia siku ya wanawake inatoa fursa ya kujadili masuala hata yasiyo ya wanawake ilikuboresha afya,hivyo unapozunguza hili si afya ya uzazi tu bali hata magonjwa kama kansa na huduma mbalimbali ambazo mama na kijana wanatakiwa kuzipata
“Ni lazima kijana anapokuwa kwenye balehe apate ujumbe huu wa Afya ya uzazi na kuepuka njia zisizo sahihi za kujamiana,”Bundala
Mratibu wa Kitaifa Masuala ya Afya ya uzazi kwa Vijana na Jinsia kutoka Wizara ya Afya Gerald Kiwele
Amesema serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha ushiriki na ushirikishwaji wa wanaume katika masuala ya afuo na uzazi uli uzae matunda.
Amesema wanaume wakishiriki ipasavyo itasaidia wanawake wajawazito na wenye watoto kuboresha afya zao kwani watachukua jukumu kama akina baba wa familia na hii itaonyesha kazi kubwa ilivyofanyika kwa ufanisi mkubwa.
“Kuna muda tunawambia akina mama tunapotoa huduma kuwa tumia vyakula fulani ambavyo vinahitaji fedha hivyo ni lazima baba atatoa fedha hiyo ilikusaidia kuboresha Afya ya mama na mtoto hivyo kupitia mwongozo utakaotolewa utaboresha maisha na utaleta mabadiliko katika jamii na kuwepo kwa ushiriki mkubwa wa wanaume na tutaweza kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi,” Kiwele
Kiwele amesema huduma zinazotolewa mwisho wa wiki zimelenga kuwapa uhuru vijana kujieleza juu ya vile walivyonavyo kwani wengi walikuwa wakiogopa kwenda kwenye hospitali siku za kazi wakihofia kukutana na ndugu zao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Utafiti MST, Esther Lubambi ameiomba serikali kuisaidia Marie
Stopes kupata mwongozo utakaosainiwa ambao uko tayari kuhakikisha wanaume wanashiriki kwenye suala la Afya ya uzazi ili utekelezaji wake uanze na uje kuwavutia wanaume kushiriki kikamilifu.
Pia amesema sasa hivi wamekuja na mpango mkakati utakaomsaidia mwanamke anapokuwa kwenye hedhi kuepuka yale maumivu na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli zake na hata pale anapofikia ukomo basi kupitia mpango huo kutamfanya mwanamke afurahie ukomo huo na kuendelea na shughuli za uzalishaji.