Na Mwandishi Wetu – Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda ya Zanzibar, Dkt. Fatma Khamis, amewataka wenye viwanda kutumia mbinu ya maboresho endelevu KAIZEN ili kuweza kuhimili ushindani na hatimaye kukuza Uchumi wetu .
Akizungumza Mapema leo kwenye Shindano la 9 la Tuzo za Kaizen lililofanyika Makumbusho ya Taifa jjini Dar es salaam Dkt. Khamis amesisitiza kuwa Kaizen husaidia kupunguza makosa na kasoro, na hivyo kuleta bidhaa na huduma bora.
“Katika mazingira ambapo wafanyakazi wanahimizwa kutafuta na kutekeleza maboresho, motisha yao na ushiriki wao huongezeka.
Aidha Dkt. Khamis ameziagiza sekta za ndani kukubali mabadiliko katika uzalishaji ili kubaki katika ushindani.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Ushirikiano la Kimataifa la Japani (JICA) nchini Tanzania, ARA Hitoshi, ameeleza kuwa Kaizen ni neno la kijapani ambalo linamaanisha mbinu m mpya ya menjimendi huku maana yake halisi ikiwa ni uboresahj endelevu.
“Kaizen inahusisha juhudi za kudumu za kuboresha mifumo ya biashara, huduma, na michakato. Mfano mzuri ni kampuni ya Kioo Limited, mshindi wa Tuzo ya Kaizen ya Tanzania mwaka 2021. Tangu kuanzisha Kaizen, kampuni hiyo imeongeza uzalishaji wa paleti kwa 50%, kupunguza taka kwa 10%, na kupunguza makosa kwa 24%,” alisema.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Kaizen kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Richard Pwereza, , amesisitiza kuwa Kaizen ni muhimu sio tu kwa biashara za binafsi bali pia kwa taasisi za umma.
“Upanuzi wa utekelezaji wa Kaizen husaidia kujenga mazingira bora ya maendeleo ya viwanda, na kuunga mkono ukuaji wa uchumi wa Tanzania,” amesema.
Kadri Tanzania inavyoendelea kukumbatia Kaizen, wadau wa viwanda wana matumaini kuwa utekelezaji wa mfumo huu kwa upana wake utachochea biashara za ndani kuelekea tija ya juu na ushindani wa kimataifa.