
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Christian Paul Makonda akiakbithi nishati hiyo kwa mama lishe na baba lishe hao mkoani Arusha leo .
Happy Lazaro,Arusha .

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda akizungumza katika hafla hiyo ya kukabithi nishati hiyo jijini Arusha.
……
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda kwa niaba ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekabidhi mitungi ya Gesi 1000, kwa Umoja wa Wajasiriamali wanaopika chakula Mkoani Arusha (Mamalishe na Babalishe), akiwasihi kuendelea kumuombea kheri kutokana na mapenzi yake makubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Kama yalivyo malengo ya serikali kuwa kufikia 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, Mhe. Makonda wakati wa makabidhiano hayo, ametangaza kuwa hivi karibuni mitungi mingine 1,000 itakabidhiwa kwa wajasiriamali hao, akisema mkakati wa mkoa wa Arusha ni kuhakikisha kuwa Wajasiriamali wote wa chakula mkoani hapa wanatumia nishati safi ya kupikia kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Matumizi ya nishati chafu ya kupikia (kuni na mkaa) kulingana na Rais Samia yana athari mbalimbali za kiafya zinazosababisha kudhoofika kwa mfumo wa upumuaji kwa wanawake, athari za kimazingira zinazotokana na uharibifu na upotevu wa misitu zinazochangiwa na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa, athari za kijamii kama vile ukatili wa kijinsia pamoja na athari za kielimu na kiuchumi kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa.
Nao baadhi ya Mama lishe na Baba lishe hao wamemshukuru Rais Samia kwa namna ambavyo amewajali na kuwakumbuka kwa kuwapatia nishati safi ya kupikia huku wakiahidi kuendelea kutunza mazingira kama yalivyo malengo ya serikali .
“Kwa kweli tunamshukuru sana Rais Samia kwa kutupa hii mitungi kwani jambo hili ni kubwa sana na tunamwahidi kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wenzetu kuhusu matumizi ya ya nishati safi na kuacha kukata miti hali.ambayo inachangia uharibifu wa mazingira. “wamesema .