Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Iddi Suwedi akizungumza na Mawakala wakati alipotembelea moja Kati ya Vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura Shehia ya Kwalinatu Wilaya ya Mjini Unguja ili kutatua Changamoto Zilizojitokeza.
Na Rahma Khamis Maelezo
Jumla ya wananchi wapiga kura wapya 9755 wanatarajiwa kuandikishwa katika daftari la wapiga kura Wilaya Mjini ili kupatiwa vitambulisho vya kupigia kura.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jaji Aziza Iddi Suwedi ameyasema hayo Skuli ya Sekondary Mpendae Wilaya ya Mjini wakati akitembelea vituo vya kuandikisha wapia kura wapya awamu ya pili ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea vituo hivyo
Amesema kuwa idadai hiyo inatokana na sensa ya watu iliyofanyika mwaka uliyopita hivyo kila mwananchi mwenye sifa ana haki ya kujiandikisha katika daftari hilo ili kupata haki yake msingi itakayomuwzesha kupiga kura.
Aidha amewanasihi wananchi Wilayani humo kuendelea kujitokeza kujiandikisha na kwa wale ambao wamepoteza ama kutaka kuhamisha taarifa zao kufika Tume ya Wilaya husika kwa ajili ya kupatiwa huduma stahiki.
Akizungumzia changamoto zilizojitokeza vituoni humo Jaji Aziza amesema kuwa kuna baadhi ya wananchi vidole vyao kutosoma lakini tayari wamesharekebishwa na zoezi linaendelea bila ya matatizo.
Wakuu wa Vituo Wilayani humo wamesema kuwa tangu kufunguliwa kwa vituo hivyo wananchi wamejitokeza kwa wingi na hali inaendelea vizuri kwani Amani na Utulivu umetawala vituoni humo.
Nae Mwananchi Mkaazi wa Magomeni Jogha Issa Muhamed amewashauri vijana wenzake ambao wana sifa na bado hawajajiandikisha kujitokeza kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura
“Kujiandikisha ni muhimu na haki ya kila mwenye sifa kwani itatusaidia kushiriki kupiga kura”,alifahamisha Mwananchi huyo,
Zoezi la uandikishaji daftari la wapiga kura wapya limeanza leo Mach 15/2025 na litaendelea hadi Mach 17 mwezi huu.
Katika ziara hiyo vituo mbalimbali vimetembelewa ikiwemo Shehia ya Mpendae,Magomeni, Miembeni, Migombani,Muembemadema,Jang’ombe, na Kwahani.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali wa Wilaya ya Mjini waliojitokeza katika Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura Wapya Shehia ya Kwalinatu Mkoa wa Mjini Mgharibi Unguja.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Iddi Suwedi akizungumza na Mawakala wa Vyama vya Siasa wakati alipotembelea moja Kati ya Vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura Shehia ya Kwahani Wilaya ya Mjini Unguja ili kutatua Changamoto Zilizojitokeza.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Iddi Suwedi akizungumza na Mawakala wa Vyama vya Siasa wakati alipotembelea moja Kati ya Vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura Shehia ya Kwahani Wilaya ya Mjini Unguja ili kutatua Changamoto Zilizojitokeza
Wananchi mbalimbali wakiwa katika Foleni katika Shehia ya Migombani kuelekea kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura wapya katika Zoezi la Uandikishaji Lililoanza Wilaya ya Mjini Unguja
Karani Undikishaji akimsajili Mwananchi aliefika kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura Shehia ya Migombani katika Zoezi la Undikishaji lililoanza Wilaya ya Mjini Unguja.
Wananchi mbalimbali wakiwa katika Foleni katika Shehia ya kuelekea kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura wapya katika Zoezi la Uandikishaji Lililoanza Wilaya ya Mjini Unguja
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Iddi Suwedi akimsikiliza Mkuu wa Kituao Cha Uandikishaji Shehia ya Matarumbeta Ali Salim Mbuguni wakati alipofanya ziara kutembelea Vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura katika Wilya ya Mjini Unguja.