MBUNGE WA Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akiwa na walimu na wanafunzi wakionesha vifaa vilivyotolewa kwaajili ya Shule za Msingi Dodoma wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa mbalimbali vya elimu yakiwemo madaftari kwa Shule zote za Msingi za Jiji la Dodoma iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mazengo.


MBUNGE WA Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Mhe.Anthony Mavunde, akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa vifaa mbalimbali vya elimu yakiwemo madaftari kwa Shule zote za Msingi za Jiji la Dodoma iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mazengo.




Baadhi ya Walimu, Wanafunzi na Wazazi waliojumuika na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Mhe.Anthony Mavunde, kwenye hafla ya ugawaji wa vifaa mbalimbali vya elimu yakiwemo madaftari kwa Shule zote za Msingi za Jiji la Dodoma iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mazengo.



MBUNGE WA Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akitoa mkono wa pongezi kwa walimu waliowahi kumfundisha wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa mbalimbali vya elimu yakiwemo madaftari kwa Shule zote za Msingi za Jiji la Dodoma iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mazengo.


MBUNGE WA Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akikata utepe wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa mbalimbali vya elimu yakiwemo madaftari kwa Shule zote za Msingi za Jiji la Dodoma iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mazengo.

MBUNGE WA Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini,Mhe. Anthony Mavunde, akiwa na walimu na wanafunzi wakionesha vifaa vilivyotolewa kwaajili ya Shule za Msingi Dodoma wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa mbalimbali vya elimu yakiwemo madaftari kwa Shule zote za Msingi za Jiji la Dodoma iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mazengo.

MBUNGE WA Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini,Mhe. Anthony Mavunde,akiwa katika picha na Wanafunzi mara baada ya hafla ya ugawaji wa Vifaa vya Masomo kwa Watoto Yatima na Watoto waishio mazingira magumu wa shule za Msingi jijini Dodoma iliyofanyika leo Machi 19,2025 katika Shule ya Msingi Mazengo.





MBUNGE WA Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini,Mhe. Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya ugawaji wa Vifaa vya Masomo kwa Watoto Yatima na Watoto waishio mazingira magumu wa shule za Msingi jijini Dodoma iliyofanyika leo Machi 19,2025 katika Shule ya Msingi Mazengo.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
MBUNGE WA Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini,Mhe. Anthony Mavunde, ameitaka Jamii kupunguza umimi na ubinafsi na badala yake wawasaidie watu wenye uhitaji hasa Wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu na yatima ili nao waweze kufikia malengo yao.
Mavunde ametoa wito huo leo Machi 19,2025 katika Shule ya Msingi Mazengo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa mbalimbali vya elimu yakiwemo madaftari kwa Shule zote za Msingi za Jiji la Dodoma.
Mavunde amesema nia yake nikuona wanafunzi waishio mazingira magumu pamoja na yatima wanapata Elimu bora na kuwa na vifaa vyote vya kujifunzia sawa na wanafunzi wengine wenye uwezo .
” Kwaniaba ya shule zote zilizopo Dodoma jiji ninamkabidhi mkuu wa kamisheni wa Elimu za msingi Dodoma madaftari 10,000 ambayo yanakwenda kugaiwa kwa watoto yatima na watoto waishio mazingira magumu.
“Kipaumbele changu kikubwa kama MBbunge wa Dodoma Mjini ni katika suala la Elimu,katika sekta ya Elimu tunazidi kuboresha ili watoto wetu wazidi kusomea katika mazingira bora na kwawale wanao nifuatilia toka zamani na kunijua vizuri wanaelewa namna gani nimekuwa nikiipa Elimu kipau mbele sifanyi haya kwa kuhitaji kura kwakuwa huu ni mwaka wa uchaguzi misaada hii naitoaga toka zamani na ukiangalia niliyowapa misaada hii ni watoto yatima ambao hawana wazazi kwahiyo hawana wa kumshawishi anipigie kura”,amesema Mavunde.
Akijibu yale yaliyowasilishwa katika risala na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mazengo Mwl.Rehema wakihitaji kujengewa uzio wa shule hiyo ili kutenganisha mipaka ya shule na makazi ya wananchi ,Mhe. Mavunde ameahidi kuwa atashirikiana na wanafunzi wote waliohitimu katika shule ya msingi Mazengo kujenga uzio wa shule hiyo pamoja na kuwajengea uwanja wa michezo na kufanya ukarabati wa shule hiyo.
Pia ameongeza kuwa atachangia matofali 5,000 kwa ajili ya uwanzishaji wa ujenzi wa uzio huo huku akisema kuwa serikali itashirikishwa mara baada ya wao kuonesha juhudi zao binafsi.
“Nimemwambia Mwalimu mkuu aende idara ya mipango awalete wataalamu waoneshe mipaka ya shule ili tuweze kuanza ujenzi wa fensi,na mimi katika hili ntajitolea matofali 5,000 pamoja na kuhakikisha nawahamashisha walewote waliyo hitimu shule hii ili tushirikiane kujenga fensi hii,pia mmeomba suala la viwanja vya michezo mwezi ujao nitawajengea uwanja wa netball na wiki hii ntawawekea goli za vyuma na nyavu zake katika uwanja wa mpira wa miguu”,amesema.
Akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwl.Rehema amesema shule ya msingi mazengo inajumla ya wanafunzi 8009 ambapo wavulani ni 390 na wasichana ni 419 huku walimu wakiwa ni 25 kati yao wakike ni 21na wakiume 3.