Mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali pamoja na radi imeezua mapaa ya Nyumba pamoja na kuharibu miundombinu ya umeme katika Manispaa ya Musoma Mkoani mara.
Wakizungumza kwa nyakati Tofauti baadhi ya wakazi katika Manispaa hiyo wamesema Mvua hiyo ulivuma upepo mkali Majira ya sanne usiku nakuanza kunyesha Mvua hivyo kusababisha Nyumba kuzaliwa.
Wakazi hao wameiomba mamlaka kuangalia kwa kina upepo huo huenda kikawa nikimbunga ambacho kimetokea na kuezua eneo moja linalofanana.
“Hiki nikimbunga hakuna upepo wa kawaida wanamna hii manaa ilikuwa Ghafla halafu ikapiga radi ndio upepo ukaanza yaani hata hatuelewi huu niupepo wa namna gan”Alisema Athuman Odhiambo mkazi katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma BW Juma Chikoka amesema hakuna kifo katika tukio hilo bali kuna majeruhi ambao wametibiwa na kuondoka na Taarifa za Kamili zitatolewa huku akiwataka wananchi kushikamana nakushrikiana katika kipindi hiki.