NJOMBE,Wakati mwezi wa funga ukielekea ukingoni ,Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Njombe imefutulisha watu zaidi ya 1500 wakiwemo madereva bodaboda,bajaji, wafanyabiashara ,viongozi wa dini na serikali na kisha kutumia fursa hiyo kutoa elimu ya kodi kwa ajili ya ustawi wa nchi.
Specioza Owure ambae ni meneja wa TRA mkoa wa Njombe amesema mamlaka imeamua kutoa iftar hiyo kama sadaka kipindi cha mfungo jambo ambalo limekwenda sambamba na utoaji wa msaada wa chakula kwa wenye uhitaji ikiwemo Sukari,Mchele,Unga wa Ngano,Mafuta ya kupikia ,Tende ,Chumvi,viazi na Tambi
Kwa upande wake mgeni rasmi wa iftari hiyo Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameipongeza mamlaka hiyo kwa kutoa sadaka hiyo na kugusa makundi mblimbali hususani maafisa usafirishaji ambao amesema ndiyo wana jukumu kubwa la kulinda usalama wa nchi kwasababu wao ndiyo wanapokea na kusafirisha watu.
Mtaka ametua mwanya huo pia kuwataka wakazi wa Njombe kuacha tabia za mauaji ambayo kwa koasi kikubwa yanafanywa na ndugu kwa shinikizo la visasi na zuruma.
Awali shekh wa mkoa Rajab Msigwa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Deo Sanga wameendelea kuhimiza ulipaji kodi kwa kuwa ni miuongozi ya dini na serikali kwa ajili ya maendeleo ya taifa lolote.




