Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Kituo cha Afya cha Mama Ngoma kilichopo Kwakoa Mwanga Mkoani Kilimanjaroa Machi 25, 2025. Kushoto kwake ni mmiliki wa kituo hicho Profesa Twalib Ngoma na kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Kituo cha Afya cha Mama Ngoma kilichopo Kwkoa Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Machi 25, 2025. Kulia ni Mbunge wa Mwanga Joseph Tadayo, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga Mwanahamisi Mnkunda na wa pili kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Mercy Mollel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Profesa Twalib Ngoma (wa pili kulia) alipozindua Kituo cha Afya cha Mama Ngoma kilichopo Kwakoa Mwanga mkoani Kilimanjaro, Machi 25, 2025. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea Kituo cha Afya cha Mama Ngoma kilichopo Kwakoa Mwanga mkoani Kilimanjaro baada ya kukizindua , Machi 25, 2025. Kushoto kwake ni mmiliki wa kituo hicho, Profesa Twalib Ngoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha tuzo aliyokabidhiwa na Profesa Twalib Ngoma (kulia) ya kutambua mchango wake katika kuimarisha huduma za Afya nchini wakati alipozindua Kituo cha Afya cha Mama Ngoma kilichopo Kwakoa Mwanga mkoani Kilimanjaro, Machi 25, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)