

NA DENIS MLOWE IRINGA
KATIBU wa NEC Itikadi Mafunzo na Uenezi Taifa wa Ccm , Amos Makala amewataka watetezi wa haki za binadamu kujitokeza kumtetea Katibu Mwenezi wa Bawacha Taifa, Sigrada Mligo aliyepigwa na mlinzi wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche kwani kitendo hicho ni unyanyasaji wa kijinsia.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa mjini Mafinga mkoani Iringa, CPA Makala alisema ni wakati sasa wa wanaharakati kujitokeza kumtetetea mwenezi wa Bawacha kwani ni kitendo ambacho kimefanywa na wapinzani ikiwa ni moja ya njia ya kuelimisha jamii kwamba wako kwa ajili ya
Kuvuruga amani kwa kitendo kilichofanywa na mlinzi huyo.
CPA Makala alitumia mkutano huo kufanya harambee ya kumchangia Sigrada Mligo matibabu ambapo jumla ya sh. Milioni 1.5 zilichangwa ambapo kati ya hizo Mnec Salim.Abri alichangia milioni 1 kwa ajili ya matibabu ya mwenezi wa Bawacha Taifa.
Makala alisema kwamba kama mwenezi amelazimika kuomba wananchi wamchangie ili kutimiza 4R za Rais Samia kuonyesha upendo kwa mwenezi mwenzake ambaye alipigwa sana na mlinzi wa Heche hali inayoonyesha kwamba chama hicho kina mgogoro ndani yake.
Alisema kama mwenezi wamemchangia Sigrada ana aliwapa maagizo viongozi wa ccm mkoa wa Njombe kumtembelea na kumjulia hali mwenezi huyo na yeye kumpigia simu kumjulia hali.
‘Nimewaagiza viongozi wa Ccm kufika kwa Nyumbani kwa Sigrada na kumjulia hali huku wakiwataka watanzania kuendelea kudumisha amani badala ya kuendekeza ugomvi na vurugu” Alisema
Aliongeza kuwa CCM wanalaani vikali kitendo hicho na wanamtakia uponyaji wa haraka Sigrada Mligo, na tunahimiza viongozi wa Chadema kuwa mstari wa mbele kulaani vitendo vya unyanyasaji ndani ya chama chao,
Makalla, ambaye pia amepewa uchifu na wazee wa kimila wa Kihehe na kupewa jina jipya la Mwalamnila Mlongahilo, likimaanisha msema kweli kwa makini
Aliipiga. Vijembe kauli ya Chadema ya No Reforms No Election kwa kuelezea namna Serikali ya Dk Samia Suluhu Hassan ilivyoyafanyia kazi maombi ya wadau wa siasa kuhusu sheria za uchaguzi.