Wataalamu wa afya kutoka Mikoa ya Iringa na Njombe, wanaohudumiwa na MSD Kanda ya Iringa wametakiwa kufanya maoteo ya bidhaa za afya kwa usahihi, ili kuimarisha mnyororo wa upatikanaji bidhaa za afya kwenye mikoa hiyo.
Rai hiyo imetolewa hii leo Mkoani Njombe na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Eng.Joseph Mutashubirwa wakati akifungua kikao cha wateja na wadau wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Iringa, kilichokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja mafanikio, changamoto na fursa zilizizopo, ili kuimarisha mnyororo wa bidhaa za afya.
Eng. Mutashubirwa amewasisitiza wataalam hao kutunza na kulinda vifaa tiba ili vidumu kwa muda mrefu, na kuleta tija kwa wananchi.
Awali, akitoa salamu za utangulizi Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Iringa, Lucas Guta amesema wameona ni vema wakikaa na wateja na wadau kuzungumza juu ya huduma wanazozitoa kama zinakidhi mahitaji yao au hazikidhi ili kuweza kuzifanyia maboresho kwa lengo kuimarisha afya za wananchi.
Guta amewataka wateja hao kujadili changamoto zilizopo kwa uwazi Ili zipatiwe tatuzi, huku akiwakumbusha kuweka mikakati mathubuti ya ulipaji madeni yao MSD, ili mnyororo wa bidhaa za afya usikatike.
Akizungumza kwaniaba ya Washiriki hao, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Juma Mfanga ameipongeza MSD kwa maboresho ya huduma zake, hasa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, huku akiitaka MSD kufanyia kazi changamoto chache zilizobakia