Afisa Rasilimali watu mkoa wa Dodoma Coletha Kiwale akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo kwenye Iftari iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo
Mkurugenzi wa Biashara wakala wa vipimo Kareem Mkorehe akizungumza kwenye Iftari iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo
Mjumbe wa bodi Wakala wa Vipimo CPA Swelehe Chindoma akizungumza kwenye Iftari iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo.
Watumishi wa ofisi ya Wakala wa Vipimo kwenye Iftari iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Afisa Rasilimali watu mkoa wa Dodoma Coletha Kiwale amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuwawezesha wafanyakazi kuwa na mazingira bora ya kufanyia kazi.
Bi. Kiwale ametoa pongezi hizo Jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo kwenye Iftari iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo kwa lengo la kupata dua ambayo itafungua mafanikio waliyoyapata kukamilisha ujenzi wa jengo lao la makao makuu.
“Amekuwa akitupatia vitu mbalimbali ikiwemo stahiki zinazoendana na maslahi ya kifedha lakini pamoja na kututengenezea makazi au majengo ambayo yanatufanya tuweze kufanya kazi zetu kwa kwa utulivu,”amesema.
Aidha, amewapongeza kwa ujenzi wa jengo lao jipya ambapo amesema kuwa changamoto za vipimo zitaenda kutatuliwa kwa ujenzi wa jengo hilo ambalo litawapa watumishi nafasi nzuri ya kufanya kazi pamoja na kuhudumia vyema wateja.
“Na nipende kusema tu kwamba Wakala wa Vipimo wamekuwa wakiendelea kutatua changamoto za vipimo kwa walaji kwa nyakati zote, siyo kwamba walikuwa hawafanyi lakini kwa changamoto ambazo zimejitokeza tumeweza kuzitatua pamoja na zile ambazo zitajitokeza tutashirikiana nao kuzitatua”, amesema.
Naye Mjumbe wa bodi Wakala wa Vipimo CPA Swelehe Chindoma amesema Wakala wa Vipimo ina shughuli ya kusimamia vipimo vyote nchini hivyo dhamira yao ni kuhakikisha wanampatia mlaji haki yake kutokana na kipimo stahiki.
“Ni dhambi kubwa kupunja kipimo kwani hata vitabu vya dini (Biblia na Qur’an) vinakumbusha waumini umuhimu wa vipimo sahihi hivyo nj jukumu letu kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wananchi,”amesema.
Amesema pia sheria zinatoa adhabu kwa wale ambao wanapunja vipimo, hivyo wanashauriwa kutenda haki na anayepaswa kupata kilo mmoja basi apewe sawa na thamani ya fedha ambayo ameilipa.
Kwa upande wake msemaji wa shekh wa mkoa wa Dodoma Sheikh Ahmad Said kwa niaba ya shekh wa Mkoa wa Dodoma amesema ofisi hiyo inafanya kazi ya kurekebisha tabia ya baadhi ya watu wenye nia ya kuwadhurumu wengine kwa njia ya vipimo
Awali, Mwenyekiti wa CPCT Dodoma, Mch. John Maliga akisema ujenzi wa jengo hilo utaenda kupunguza dhuruma kwa watanzania ikiwa wafanyakazi watatenda haki bila kuhofia cheo na wadhifa wa mwanadamu kwa kupokea rushwa ambayo ni kinyume na maagizo ya mwenyezi Mungu.