Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Juma Makungu Juma (katikati)akiwa pamoja na Viongozi na Wananchi mbalimbali wakiomba Dua katika kaburi la Marehemu Maalim,Hamid Ameir Ali .Ikiwa ni katika wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar .hafla iliofanyika Donge Vijibweni Wilaya Kaskazini B Unguja.Dua ilioongozwa na Sheikh kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Mziwanda Ngwali Ahmed.
PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR
…….
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hunafanya dua maalumu ya kuwaombea waasisi na Viongozi wa Mapinduzi waliotangulia kila mwaka ili kukumbuka mazuri waliyoyaacha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Juma Makungu Juma ameyasema hayo huko Donge Vijibweni Wilaya ya Kaskazini B’ wakati wa dua maalumu ya kumuombea Marehemu Hamid Ameir Ali ikiwa ni kuelekea siku ya mashujaa.
Amesema kuwa wazee hao wamejitolea kwa hali na moyo mmoja kuhakikisha wananchi wanankua huru hivyo ni vyema kujifunza uzalendo na usiri uaotokana na viongozi hao kwani walilua na usiri mkubwa ambao umepelekea kupata uhuru na kuleta maendeleo katika nchi.
“Hapa vijana tunafundishwa kua na usiri tunapoambiwa jambo hatupaswi kumwambia mtu yote haya ni mafunzo tuliyoyapata kutoka kwa wazee wetu” alikumbusha Naibu Waziri.
Ameongeza kuwa wazee hao wameondoka wameacha alama nzuri hivyo ipo haja kwa vijana kujitahidi kutenda mema ili kuacha historia njema wakati watakapoondoka duniani.
Aidha ameipongeza Ofisi ya Mufti kwa kuandaa shughuli hiyo kwani kila inapofanyika dua hizo hushiriki kuhakikisha shughuli inakwenda vizuri
Nae Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Sururu Juma Sururu amefajisha kuwa huo ni uratibu maalumu ambao umepangwa na Serikali kufanya hivyo kila mwaka .
Siku ya mashujaa huadhimishwa kila ifikapo Aprili 7 ambapo huambatana na wiki ya mashujaa kwa kuzuru makaburi ya waasisi navoongozi mbalimbali wa mapinduzi kuwaombea dua hadi kufikia kilele chake.

Sheikh kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Mziwanda Ngwali Ahmed akizungumza kuhusiana na kuwaombea Dua waliotangulia na Fadhila zake katika Msikiti wa Donge Vijibweni katika hafla ya kumuombea Dua Marehemu Maalim,Hamid Ameir Ali aliezikwa katika Kijiji hicho .Ikiwa ni katika wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar .hafla iliofanyika Donge Vijibweni Wilaya Kaskazini B Unguja.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Juma Makungu Juma (kulia)akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Sururu Juma Sururu katika Kisomo maalum Cha Khitima ya Kumuombea Marehemu Maalim,Hamid Ameir Ali .Ikiwa ni katika wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar .hafla iliofanyika Donge Vijibweni Wilaya Kaskazini B Unguja.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Juma Makungu Juma akizungumza na Waumini wa Dini ya kiislamu kuhusiana na kuwaenzi Viongozi waliotangulia na kufuata Mwenendo wao katika hafla ya Kumuombea Dua Marehemu Maalim,Hamid Ameir Ali .Ikiwa ni katika wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar .hafla iliofanyika Donge Vijibweni Wilaya Kaskazini B Unguja.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Juma Makungu Juma akimkabidhi Kiongozi wa Familiaya ya Merehemu Maalim Hamid Ameir Ali Bahasha ya Sadaka ya Ubani iliotolewa na Serikali katika hafla ya Kumuombea Dua Marehemu huyo .Ikiwa ni katika wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar .hafla iliofanyika Donge Vijibweni Wilaya Kaskazini B Unguja.