Na Prisca Pances
SERIKALI ameahidi kuchangia kiasi cha Sh. milioni 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Saranga, kilichopo katika Wilaya ya Ubungo,mkoa wa Dar es Salaam.
Ahadi hiyo imetolewa jana Aprili 9,2025na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo, hususani miradi katika sekta ya afya, elimu, na maji.
“Mimi kama Mkuu wa mkoa ninayependa siasa za vitendo naelekeza kuwa mpaka kufikia ijumaa kuu milioni 100 zitakuwa zimekwisha ingizwa kwenye akaunti yenu ilikumalizia ujenzi pamoja na kuezeka paa ilikituo hiki kiweze kufanya kazi kwa kuwahudumia wananchi wa eneo hili,”amesema Chalamila.
Aidha, Chalamila amewataka wananchi kuchagua viongozi wanaofanya siasa za vitendo na si maneno ili kuleta maendeleo endelevu katika jamii.
Kuhusu kero ya barabara Chalamila alisema lazima utaratibu wa ufuatwe ili kuhakikisha hakuna malalamiko kutoka kwa wananchi.
“Tulipeleka suala hili benki ya Dunia kuwa mnahitaji kujengewe kilometa 10 lakini walikataa kwasababu mradi huo ungechukua makazi mengi ya watu na sharti walilotupa ni sisi kulipa fidia kwasababu wao hawawezi,”amesema Chalamila.
Ameongeza,”Katika suala hili tayari tumekwisha fanya tathimini ya watu wanagapi watalipwa na si chini ya bilioni 7 zitakazotumika kulipa fidia hizo,kwa wakati huu tupo mbioni kutangaza nafasi za kazi kwa mkandarasi ilikazi ianze mara moja,”
Amesema mbali na barabara ya Saranga, zingine zilizopo kwenye mradi ni kilometa 255 zinazosimamiwa na TARURA zitagharimu kiasi cha Sh bilioni 890.