Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,akishuhudia utilianaji Saini wa Makubaliano kati ya Wizara ya Kilimo na Mkataba na Kampuni ya United Capital Tertelizer ya nchini Zambia kwa ajili ya Mauziano ya Mbolea aina ya NPK kwa ajili ya wakulima wa Zao la Tumbaku,hafla iliyofanyika leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma.
Na Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Kilimo imesaini Mkataba na Kampuni ya United Capital Tertelizer ya nchini Zambia kwa ajili ya Mauziano ya Mbolea aina ya NPK kwa ajili ya wakulima wa Zao la Tumbaku.
Hayo yameelezwa leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma na na Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe mara baada ya kushuhudia utilianaji Saini ya Makubaliano hayo ambapo amesema kuwa ndani ya makubaliano hayo yapo makubaliano ya kujenga kiwanda cha Mbolea hapa nchini lengo ni kurahisisha upatatikanaji wa Mbolea kwa wakulima wa zao hilo.
Waziri Bashe amesema wamekubaliana na UFCL kwa ajili ya kujenga Kiwanda cha kuzalisha tumbaku ambapo amedai mchakato wa awali tayari umeishafanyika na shughuli zingine za utekelezaji zinaendelea.
Amesema wanaangalia eneo ambalo litawekwa Kiwanda hicho huku akidai watashirikiana kwa pamoja na sekta binafsi na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC).
“Hii ni sehemu ya utekelezaji na Mheshimiwa Rais na mahusiano yetu hayatakuwa ya mwaka mmoja yatakuwa kwa zaidi ya miaka mitatu,”amesema Waziri Bashe.
Aidha,Waziri Bashe amewapongeza wakulima wa zao la tumbaku kwa kazi nzuri wanayofanya pamoja na vyama vya ushirika ambapo amedai Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano na wataufungua mpya msimu wa zao hilo hivi karibuni.
Amesema wamefunga msimu wa Serengeti na wamepata zaidi ya kg milioni 2.2 na bei ya wastani ikifika zaidi ya Dola 2.5 kwa wakulima wa Serengeti ambapo amedai uzalishaji huo ni mkubwa.
Ametaja sababu ya ongezeko la uzalishaji ni kutokana na pembejeo kwenda kwa wakati kwa wakulima wa maeneo hayo.
Katika hatua nyingine,Waziri Bashe ametoa wiki kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Joel Laurent kuhakiki majina ya wakulima wa zao la tumbaku ili waweze kupatiwa ruzuku zao.
Amesema tayari Serikali imeishatoa zaidi ya Sh bilioni 13 lakini kumetokea changamoto ya majina kwa wakulima.
“Nimewapa siku saba wahakiki majina ya wakulima ili wakulima wapate fedha yao ya msimu uliopita,”amesema Waziri Bashe.
Waziri huyo wa Kilimo amesema mpango wa Serikali kwenye ruzuku itaendelea kwani ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kuhusu Mbolea ya kupandia amesema tayari TFC inazo tani 14 na mbolea yote ya shambani tayari imezalishwa.
“Vyama vya ushirika andaeni maghala ya kuhifadhi Mbolea ya mashambani.Nitumie Nafasi hii kuwashukuru Serikali itaendelea kuwa pamoja na nyie kwa kuwalinda,”amesema Waziri Bashe.
Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,akizungumza mara baada ya kushuhudia utilianaji Saini ya Makubaliano kati ya Wizara ya Kilimo na Mkataba na Kampuni ya United Capital Tertelizer ya nchini Zambia kwa ajili ya Mauziano ya Mbolea aina ya NPK kwa ajili ya wakulima wa Zao la Tumbaku,hafla iliyofanyika leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,akishuhudia utilianaji Saini wa Makubaliano kati ya Wizara ya Kilimo na Mkataba na Kampuni ya United Capital Tertelizer ya nchini Zambia kwa ajili ya Mauziano ya Mbolea aina ya NPK kwa ajili ya wakulima wa Zao la Tumbaku,hafla iliyofanyika leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma.