Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa alipowasili kwenye ukumbi wa Jiji uliopo kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma kufungua Mkutano wa 15 wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TOA), Aprili 14, 2025. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachwene na kulia ni Mwenyekiti wa TOA Taifa, Albert Mtovelwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa (kushoto) alipotembelea mabanda ya maonesho kabla ya kufungua Mkutano wa 15 wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA), Aprili 14, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Vicky Bishubo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa serikali wa Benki ya NMB wakati alipotembelea banda la maoneho la Benki hiyo kabla ya kufungua Mkutano wa 15 wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA), Aprili 14, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa alipoingia kwenye ukumbi wa Jiji uliopo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma kufungua Mkutano wa 15 wa Taasisi ya Maboresho ya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA), Aprili 14, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipofungua Mkutano wa 15 wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA), kwenye ukumbi wa Jiji uliopo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma, Aprili 14, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)