VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika kutekeleza agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hasana la kutunza na kuhifadhi mazingira ambapo imefanikiwa kupanda miti zaidi ya mia 500 katika eneo la mnada wa mbuzi na ng’ombe uliopo katika Kata ya Zinga kwa mtoro lengo ikiwa ni kuweza kurudisha uoto wa halisi uliopotea pamoja na kupambana na wimbi la na ukataji wa miti ovyo ambao unasabisha hali ya ukame.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Stellah Msofe wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji wa miti ngazi ya Wilaya ambayo yamefanyika katika eneo la Zinga kwa mtoro ambapo amewataka wakuu wa idara, watendaji,zikiwemo taasisi binafsi kuweka mikakati ya kuhimiza suala la upandaji wa miti ili kutimiza agizo la serikali la kupanda miti milioni 1.5 kwa kila mwaka.
Alisema kwamba serikali imeamua kwenda kupanda miti katika eneo hilo la mnada wa Zinga kutokana na kubaini kwamba mazingira yake yameathirika kwa kiasi kutokana na kuwepo kwa shughuli mbali mbali za kibinadamu ikiwemo suala la uchimbaji wa mchanga hivyo wakaona kun aumuhimu mkubwa sana katika kuhakikisha anapanda miti mingi ambayo itasaidia kurejesha hali yake ya kawaida.
Naye Mkuu wa kitengo cha maliasili na mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoto Dkt. Obed Mwinuka amebainisha kwamba lengo lao kubwa ni kutekeleza kampeni ya kitaifa katika kuboresha mazingira ambapo wamefanikiwa kupanda miti ipatayo 500 katika eneo hilo la mnada wa mbuzi na ng’ombe lililopo kata ya Zinga.
Pia alisema kwamba lengo kubwa la Halmashauri ni kuhakikisha kwamba wanapanda miti mingi ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto ya ukame ambao umekuwepo katika baadhi ya maeneo na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha utunzaji wa mazingira .
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo amebainisha kwamba hadi sasa wameshafanikiwa kupanda miti zaidi ya laki saba na kwamba lengo na mikakati waliyojiwekea ni kufikia lengo la serikali la kupanda miti milioni 1.5 ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kurudisha hali nzuri ya uoto wa hasiri.

Mmoja wa wawekezaji katika mnada huo wa Zinga kwa mtoro Hassan Kashingo akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake ameahidi kushirikiana bega kw abegaa naa serikali ikiwa pamoja na kuitunza miti hiyo 500 ambayo imepandwa katika eneo hilo la mnada.