đź“Ś Atembelea miradi ya ujenzi chuoni
đź“Ś Apokea taarifa ya uendeshaji na Programu za kitaaluma
đź“ŚAzungumza na Wanafunzi
Na WMJJWM – Dar Es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesema Programu za Ubunifu, Uanagenzi na Ushauri Nasihi ni fursa ya ajira kwa vijana nchini huku akiwahimiza vijana kutumia fursa hiyo ili wanapomaliza Chuo waweze kujiajiri na kuajiri wengine.
Dkt. Jingu ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Aprili 17, 2025 kukagua maendeleo ya mradi wa jenzi wa jengo la mihadhara na utoaji huduma Chuoni hapo.
Katika ziara hii Dkt. Jingu amewasihi wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kushiriki katika programu zinazotatua changamoto mbalimbali katika jamii ili elimu waliyoipata iweze kutoa matokeo chanya katika jamii.
“Ninyi ni mainjinia wa kuleta mabadiliko katika jamii nimevutiwa sana na programu mnazoshiriki na kufanya hapa chuoni na kusema kweli ni nzuri sana” Ubunifu, Uanagenzi, Utoaji wa ushauri nasihi zote hizi ni fursa za ajira kwenu msizichukulie kimzaha” amesisitiza Dkt. Jingu.
Aidha amewaasa wanafunzi kuongeza juhudi ya kusoma zaidi ya darasani ila pia kuendana na kasi ya utumiaji teknolojia kama vile akili bandia kutoa huduma na kuwa na mahusiano mazuri na wadau wa sekta washirika ambao ni muhimu kwao.
Dkt. Jingu ameipongeza Menejimenti ya Chuo hicho kwa ubunifu katika kutoa elimu na Huduma za Kitaaluma hivyo kuendelea kwa Chuo kuonekana umuhimu wake kwa jamii na kuendelea kuwa kitovu cha ubora wa elimu na ujuzi unaoenda kutatua changamoto katika jamii na kuboresha maisha ya watanzania ambalo ndio lengo la Serikali ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pia Dkt. Jingu ametembelea mradi wa ujenzi wa ukumbi wa mihadhara na hatua za utekelezaji huku akisisitiza ubora na ukamilishwaji wa mradi kwa wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amesema Chuo kimeandaa mitaala mipya minne (4), itakayoongeza programu 15 za mafunzo katika fani mbalimbali ambapo Mitaala hiyo imepata ithibati na itaanza kutumika katika mwaka wa masomo 2025/2026.
​Â