Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli,akizungumza wakati akifungua mdahalo wa kitaifa wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Taasisi ya Kilimo Roundtable Afrika(KRTA) kwa ushirikiano na Chuo cha Uchumi na Mchongo TV uliofanyika leo Aprili 24,2025 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifungua mdahalo wa kitaifa wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Taasisi ya Kilimo Roundtable Afrika(KRTA) kwa ushirikiano na Chuo cha Uchumi na Mchongo TV uliofanyika leo Aprili 24,2025 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli,akizungumza wakati akifungua mdahalo wa kitaifa wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Taasisi ya Kilimo Roundtable Afrika(KRTA) kwa ushirikiano na Chuo cha Uchumi na Mchongo TV uliofanyika leo Aprili 24,2025 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli (hayupo pichani) wakati akifungua mdahalo wa kitaifa wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Taasisi ya Kilimo Roundtable Afrika(KRTA) kwa ushirikiano na Chuo cha Uchumi na Mchongo TV uliofanyika leo Aprili 24,2025 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema mradi wa Mashamba ya Vijana wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) umeendelea kuimarika nchini huku vijana 12 waliokuwa wakiilalamikia wizara hiyo kwenye mitandao ya kijamii kwa kutoa pesa ndogo ya kujikimu walioondolewa kutokana na kuonesha kutokuwa tayari kuwapo kwenye mradi huo.
Bw.Mweli ametoa kauli hiyo leo Aprili 24,2025 jijini Dodoma,wakati akifungua mdahalo wa kitaifa wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Taasisi ya Kilimo Roundtable Afrika(KRTA) kwa ushirikiano na Chuo cha Uchumi na Mchongo TV.
Amesema kuwa Vijana wengi wao hawakuwa na elimu ya kilimo pamoja na ardhi ambavyo vyote walipatiwa na serikali baada ya kujiunga na mradi huo.
“Niwaambie wale waliokuwa wanashinda mitandaoni 12 tumewaacha, tunaendelea na wale walio tayari tusafiri pamoja tutoke huku tuliko,vijana tufahamu nchi hii ni lazima tuijenge wenyewe na kuna fursa kwa kuwa serikali imeamua kufungua milango,”
“Tuna BBT yanasemwa maneno mengi sana na wanaosema ni wale waliochukuliwa wakipewa mashamba, mbegu, vifaa na masoko na alichukuliwa akiwa hana ajira tunawaambia lima hapa sisi tutanunua, wanasema mbona posho ndogo na huyo mtu alikuwa hana posho wala kazi sasa anaona ndogo,”amesema Bw.Mweli.
Hata hivyo amefafanua kwenye mradi huo kuna program sita ikiwamo ya kuajiri vijana waliosomea kilimo na tayari 2000 wameajiriwa kwa mkataba kupitia Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA) na wamesambazwa nchini.
“Tunawapatia pia mikopo ya riba nafuu na tumepunguza masharti magumu hakuna uwekaji dhamana zaidi ya kulipa bima ya mkopo, niwatangazia vijana wote ambao wanafanya kweli miradi ya kilimo wachangamkie mikopo,”amesema
Pia, amesema kuwa Serikali kupitia Halmashauri zimeanzisha mashamba mengine kwenye maeneo hayo kwa ajili ya vijana kufanya kilimo na hadi sasa Halmashauri 18 zina mashamba hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kilimo Roundtable Africa(KRTA),Bi. Rhoda Magoiga amesema kuwa taasisi hiyo inatekeleza mpango mkakati wake wa miaka mitano 2025-2029 unaojikita kwenye ujenzi wa sekta ya kilimo iliyo shindani, jumuishi na endelevu kutokana na sekta hiyo kubeba matumaini ya vijana, familia na jamii za vijijini na mijini.
“Miaka mitano zaidi ya wakulima 50,000 watafikiwa kupata mafunzo, mitandao ya masoko na teknolojia.”amesema Bi.Rhoda
Aidha ametaja changamoto zinazohitaji nguvu ya pamoja kukabiliana nazo kuwa kwenye sekta hiyo kuwa ni tija ndogo, upungufu wa miundombinu ya kuhifadhi na kusindika mazao, upatikanaji wa fedha za uwekezaji na ukosefu wa taarifa sahihi kwa wakati muafaka.