Mh Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga akizungumza na wananchi wa kata ya chanji manispaa ya Sumbawanga kuhusu unywaji salama wa pombe
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa SACP Justin Masija akithibitisha kutokea kwa vifo 32 vilivuotokana na unywaji wa pombe
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara kuhusu unywaji wa pombe salama
Na Neema Mtuka. Sumbawanga
Rukwa :Jeshi la polisi mkoa wa Rukwa limeanzisha kampeni maalum ya unywaji pombe salama ili kuepuka madhara yatokanayo na unywaji usiozingatia afya.
Akizungumza leo April 25 ,2025 katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na jeshi hilo katika kata ya chanji manispaa ya a Sumbawanga kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Rukwa kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Shadrack Masija amesema kuwa watu 32 wamepoteza maisha kutokana na unywaji wa pombe usiozingatia afya.
Amesema moja ya sababu kubwa ya unywaji wa pombe ni kutokula chakula na kutochagua unywaji wa pombe pamoja na afya aliyonayo mnywaji.
“Unakuta mtu anakunywa pombe na hajala chakula na madhara yake pombe ile inamletea madhara na kuchochea ugomvi usiokuwa wa lazima.”amesema Masija.
Amesema kuwa idadi hiyo ya watu 32 imethibitishwa na daktari akitolea ufafanuzi kuhusu vifo hivyo kuwa vimetokana na pombe kuzidi mwilini.
Akizungumzia kuhusu madhara ya unywaji wa pombe kamanda Masija amesema kumekuwa na wimbi la watoto wa mitaani kwa sababu wazazi/walezi wamewatelekeza watoto wao.
Pia amesema ukosefu wa malezi bora kwa watoto na lishe bora kunakotokana na kukosa chakula bora kunasababisha udumavu.
“Unywaji holela wa pombe unasababisha ngono zembe ubakaji ,ulawiti wa watoto na ukosefu wa maadili katika jamii”.
Kwa upande wake mganga mkuu wa zahanati ya kizwite Dr Simon Mjema amesema kuwa unywaji wa pombe kupitiliza imekuwa ni changamoto kwa afya familia jamii na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa unywaji wa pombe unaweza kusababisha ugonjwa wa ini ,shinikizo la damu kiharusi na hatimaye kusababisha kifo.
Aidha amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuwa na familia yenye afya njema .
Amesema pia unjwaji wa pombe unaweza kusababisha tatizo la afya ya akili kwa sababu pombe inakwenda kuathiri mfumo wa utendaji kazi wa ubongo.
Akizindua kampeni hiyo maalum mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile amewataka wananchi kuzingatia kanuni za afya na kuacha tabia ya kuwapa watoto wadogo pombe ili walale.
“Kuna tabia ya baadhi ya akina mama wanawapa watoto wadogo pombe ili walale na wao kuendelea na shughuli zao hali hiyo inasababisha udumavu na utapiamlo.”amefafanua Nyakia
Nyakia Amesisitiza kuwa ni muhimu watoto wakapewa lishe bora kwa kupewa chakula mchanganyiko na kuacha tabia hiyo ya kuwapa pombe mara Moja.
Aidha Nyakia amesema kuwa unywaji wa pombe kupindukia unarudisha nyuma maendeleo ya taifa na kuchochea umasikini kwa jamii
Naye mraibu wa pombe kutoka katika mtaa wa soweto kata ya chanji ezebio senga amesema kuwa pombe ni maisha yake hawezi kuacha.
“Siwezi kuacha pombe kwa kuwa nakunywa siwazi chochote nakunywa nalala maisha yanaendelea “amesema Senga.
Senga ametelekeza familia yake ya watoto wanne kutokana na unywaji wa pombe usiozingatia afya na malezi.
Aurelia Lunguya ni mke wa Senga anasema mume wake alianza kunywa pombe hata kabla hawajaoana na ikafikia hatua ya kuwa mlevi kupindukia.
“Hafanyi kazi ni mgomvi hajui thamani ya maisha anachojua yeye ni kunywa pombe tu ameniachia mzigo mkubwa ninalea watoto wangu mwenyewe”amesema Lunguya.Sheikh
Mohammed Abdallah amesema jamii inapaswa kumgeukia Mwenyezi Mungu na kuacha kufanya matendo mabaya ambayo hayatawapeleka peponi.