Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francisko iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican leo tarehe 26 Aprili 2025.
…..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema namna bora ya kumuenzi aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani hayati. Baba Mtakatifu Francisko ni kudumisha amani pamoja na kujali masikini.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa mazungumzo mara baada ya kumalizika kwa Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani hayati. Baba Mtakatifu Francisko iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro – Vatican. Amesema Papa Francisko alikuwa mnyenyekevu na mtu aliyefanya jitihada kubwa za utafutaji amani maeneo mbalimbali duniani na kuacha alama ikiwemo tukio la kuwabusu miguu viongozi wa Sudan ili waweze kuachana na mapigano.
Makamu wa Rais amesema kati ya nyaraka za mwisho alizosaini hayati Papa Francisko ni pamoja na barua aliyomwandikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumtakia heri ya siku njema ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika Misa hiyo ya Mazishi, Makamu wa Rais ameongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi wa Tanzania Vatican Mhe. Balozi Hassan Mwameta pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi. Swahiba Mndeme.
Misa ya Mazishi ya Papa Francisko imehudhuriwa na zaidi ya watu 250,000 ikiwemo viongozi wakuu kutoka mataifa mbalimbali duniani. Maziko ya Papa Francisko yamefanyika katika Basilika ya Maria Maggiore leo tarehe 26 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican kushiriki Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francisko leo tarehe 26 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francisko iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican leo tarehe 26 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Balozi wa Tanzania Vatican mwenye makazi yake Berlin Ujerumani Mhe. Balozi Hassan Mwamweta wakati wa Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francisko iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican leo tarehe 26 Aprili 2025.
picha mbalimbali Misa ya Mazishi ya Papa Francis