Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya siku yawafanyakazi duniani, Mei Mosi kwenye uwanja wa Bombadia Mkoani Singida, Aprili 30, 2025. Maadhimisho hayo yatafanyika kitaifa mkoani humo na Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri MKuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mary Maganga, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Zuhura Yunus, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Martha Mlata na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya, alipowasili kwenye uwanja wa Bombadia Mkoani Singida kukagua Maandalizi ya maadhimisho ya siku yawafanyakazi duniani, yanayofanyika kitaifa mkoani humo na Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete akitoa kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya siku yawafanyakazi duniani ambayo kitaifa yatafanyika kwenue uwanja wa bombadia Mkoani Singida, Aprili 30, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)