RAIS wa Msumbiji Mheshimiwa Daniel Chapo tayari amewasili Zanzibar akitokea Jijini Dar Es Salaam ambapo akiwa Zanzibar atakua na ziara fupi ya kikazi
Akiwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume amepokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Hamza Hassan Juma pamoja na viongozi wengine akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nchini Tanzania Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo
Rais Chapo atakutana na Mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi pamoja na kutembelea kituo cha Uvuvi cha Bahari kuu Fumba






