MBUNGE wa Nanyamba,Mhe.Abdallah Chikota (CCM) akichangia leo Mei 12,2025 bungeni Dodoma mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2025-2026.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MBUNGE wa Nanyamba,Mhe.Abdallah Chikota (CCM) ameishauri Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kufanya mafunzo kwa walimu waliomakazini ili kukuza utendaji wao pamoja na kuwaongezea maarifa mapya.
Akichangia leo Mei 12,2025 bungeni mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2025-2026,Mbunge huyo amesema kuna faida tano kama walimu waliomakazini watapatiwa mafunzo.
Amezitaja faida hizo ni kukuza utendaji,mtumishi kupata maarifa mapya,kukuza uhusiano,unakuza ufahamu wa kile unachokifahamu na inaongeza kipato cha utumishi.
“Nikupongeze Waziri walimu ni jeshi kubwa lazima tutafute fedha kwa ajili ya mafunzo kazini lazima wapate taarifa na maarifa mapya ili tuwe na walimu wa kisasa,”amesema Mhe.Chikota