Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB ,Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha

Mwenyekiti wa bodi ya benki ya CRDB, Dkt Ally Laay akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha



………
Happy Lazaro, Arusha
MAKAMU wa Rais Dkt.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgenirasmi kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa 30 wa wanahisa wa benki ya CRDB mei 17,jijini Arusha .
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB ,Abdulmajid Nsekela wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano mkuu wa 30 wa benki ya CRDB wenye kauli mbiu ya “miaka 30 ya ukuaji pamoja “.
Amesema kuwa , mwaka huu benki ya Crdb inasherehekea miaka 30 ya mafanikio ambapo kwa mwaka jana walilipa gawio la shs 50 huku kwa mwaka huu wanalipa 65 hiyo ni tofauti kubwa ambapo mwaka jana faida ilikuwa bilioni 450 ambapo mwaka huu ni bilioni 551 .
Amesema kuwa ,wanahisa watarajie kuangalia mafanikio ya benki yao katika zile kampuni tanzu zilizotajwa mwaka jana wakati zinaanzishwa kwani zimeanza biashara watapata fursa ya kusikiliza mafanikio ndani ya mwaka mmoja yakoje.
Ameongeza kuwa ,watapata nafasi ya kusikiliza mabadiliko ya kiteknolojia ambayo yamefanyika ndani ya mwaka mmoja katika benki yao.
Nsekela ameongeza kuwa , watapata fursa ya kusikiliza mafanikio ya mwaka jana ambayo ni makubwa na sasa mwaka 2025 robo ya kwanza imeisha na wanahisa watapata nafasi ya kusikiliza taarifa za hesabu za robo ya kwanza yenye mafanikio makubwa kwani mwaka jana desemba amana za benki ya aseti nzima ilikuwa ni trilioni 16.6 ambapo robo ya kwanza ya 2025 machi ni trilioni 17.6 .
Amesema kuwa faida ya benki ni bilioni 173 na hiyo haijawahi kutokea yapo mengi waliyofanikiwa kwani amana za wateja imekuwa mikopo.imeongezeka na pia kampuni tanzu imewagusa watanzania wengi.
Amesema kuwa,mpango wa kutanua matawi nje yanafanya vizuri ikiwemo benki ya Burundi inafanya vizuri sana na ni ya kwanza na biashara imeanza kushamiri DRC Congo walikuwa Lubumbashi ila sasa hivi wapo Kinshasa matawi matatu yanafanya kazi .na walikuwa wanafuatilia vibali vya kufungua tawi Dubai na vibali vimekamilika wanakamilisha ofisi ili kazi ianze.
Amesema mpango mkakati walionao wanaangalia nchi zote za Afrika Mashariki ambapo wanaendelea na mchakato kwani wanatarajia kwenda nchi zote za afrika Mashariki ambapo wana mpango wa kuangalia mataifa kama Dubai unaendelea.
“katika soko la hisa ukiangalia kwenye hisa inayouzika sana inayotafutwa sana bila kupatikana ni hisa za benki ya CRDB .”amesema Nsekela.
Amesema kuwa, wateja wanazidi kuongezeka kwa sababu imani ni kubwa sana ,amesema kuwa bei inaongezeka kila mwekezaji anapenda kuwekeza panapolipa na penye ufanisi tumefanya mabadiliko makubwa sana ya kiuendeshaji tumeongeza ubunifu mkubwa sana wa huduma zao na tumeboresha miundombinu yao sana kwani hata huduma zao za kidigitali zimeongezeka na matumizi yamepungua na wamejikita zaidi kufanya kazi na wadau wa kitaifa na kimatifa kwenye miradi ya kimkakati hivyo kuongeza wigo wa huduma .
Mkurugenzi wa CRDB Foundation Tulli Esther, amesema kuwa kabla ya mkutano huo benki hiyo itafanya matukio mbalimbali kwa jamii ikiwemo kukabithi madarasa maalumu katika shule ya Uswaa iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Ameongeza kuwa, benki hiyo itakabithi pia madarasa kwa shule iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha pamoja na kutoa semina kwa vijana na wanawake katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha .
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya CRDB, Dkt Ally Laay amesema kuwa, kutokana na faida hiyo bodi ya wakurugenzi imependekeza gawio la shs 65 kwa kila hisa,ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 30 ukilinganisha na gawio la mwaka jana 2024 la shs 50.