Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said ametoa wito kwa vyama vya Ushirika mkoa wa Mwanza kuendelea kutumia jukwaa la michezo mbalimbali katika kuimarisha na kujenga Ushirikiano.
Mtanda ametoa wito huo hii leo wakati akifungua bonanza la michezo kwenye uwanja wa Nyamagana lililowakutanisha vyama mbalimbali vya ushirika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Mwanza linalotarajiwa kufanyika Mei.25,Mwaka huu.
Kwa upande wake mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Mwanza Hilda Boniface amesema vyama ya ushirika mkoa wa mwanza vinajari michezo na afya kwa wanaushirika.