Programu ya ‘Be Road Safe Africa’ ni sehemu ya dhamira ya Puma Energy Tanzania ya kusaidia usalama na ustawi wa jamii, hasa jamii zilizo katika mazingira magumu na maeneo hatarishi. Kupitia mafunzo ya mbinu mbalimbali, mashindano, na uboreshaji wa miundombinu, programu hii inasaidia kuzifanya barabara zetu kuwa salama kwa watoto wa shule nchini.
Wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, kutoka kushoto, Abdulrazack Shaban Fundi (14), Nadya Salumu Abdallah (13), Munir Said Mussa (12), Agness Daud Frank (13), na Mohamed Abubakari Muhidin (13) wakimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini. Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya usalama barabarani mashuleni ilifanyika 2023 na 2024, kwa awamu ya pili mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 katika shule tano za jijini Dar es Salaam ambazo ni Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala) kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo, mahakama kifani ya watoto na mashindano ya kuchora alama za usalama barabarani.
Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, Mohamed Abubakari Muhidin (13), wa kwanza kulia, akimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini. Wakifuatilia kwa makini kutoka kulia kwake ni Agness Daud Frank (13), Munir Said Mussa (12), Abdulrazack Shaban Fundi (14) na Nadya Salumu Abdallah (13). Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya usalama barabarani mashuleni ilifanyika 2023 na 2024, kwa awamu ya pili mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 katika shule tano za jijini Dar es Salaam ambazo ni Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala) kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo, mahakama kifani ya watoto na mashindano ya kuchora alama za usalama barabarani.
Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, Munir Said Mussa (12), katikati, akimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini. Wakifuatilia kwa makini kulia kwake kushoto kwake ni Agness Daud Frank (13) na Munir Said Mussa (12), na kulia kwake ni Nadya Salumu Abdallah (13) na Abdulrazack Shaban Fundi (14). Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya usalama barabarani mashuleni ilifanyika 2023 na 2024, kwa awamu ya pili mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 katika shule tano za jijini Dar es Salaam ambazo ni Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala) kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo, mahakama kifani ya watoto na mashindano ya kuchora alama za usalama barabarani.