Serikali imekutana na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Asasi ya Kimataifa ya Water Aid lengo likiwa kuimarisha Sekta ya Maji kusonga mbele zaidi katika kutoa huduma kwa wananchi.
Kikao kimeongozwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Wizara ya Maji.
Kikao kimefanyika ikiwa ni takribani miezi miwili tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupokea tuzo ya Kinara wa Maji Afrika (Pan-African water, Sanitation and Hygiene Award) kutoka asasi ya kimataifa ya Water Aid ambayo imetambua uongozi mahiri wa Rais Mhe. Dkt. Samia katika kuboresha huduma ya maji na usafi wa mazingira nchini kwa wananchi hapa nchini.
Pamoja na hilo Mhe. Dkt. Samia katika tuzo hiyo alipewa heshima ya kuwa Mlezi wa Bara la Afrika katika Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira
Pamoja na hilo, Siku ya Maji Duniani Machi 22, Rais Mhe. Dkt. Samia alipewa tuzo ya Kitaifa ya Mageuzi katika Sekta ya Maji (Game Changer Award).
Gemma Querol Prades ambaye ni kiongozi Mkuu upande wa Maji, Usafi wa Mazingira na usafi Binafsi kutoka UNICEF katika kikao amesema serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya sekta ya maji na kwamba UNICEF ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha maendeleo zaidi yanapatikana katika huduma ya maji.