Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaosimamia masuala ya fedha na uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (17th SCFEA), uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha, ambapo alihimiza nchi wanachama kuimarisha zaidi utengamano wa kikanda ili kuharakisha maendeleo ya nchi hizo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu EI-Maamry Mwamba.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(Katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu EI-Maamry Mwamba (kulia) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Yusuf Mwenda (kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 17 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaosimamia masuala ya fedha na uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (17th SCFEA), uliotanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha, ambapo Katika Mkutano huo Ukt. Nchemba alihimiza nchi wanachama kuimarisha zaidi utengamano wa kikanda ili kuharakisha maendeleo ya nchi hizo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)