Serikali kupitia Wizara ya Maji inaendelea kuongeza jitihada za utunzaji na ulindaji wa vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwa na uhakika wa rasilimali za maji kufikisha huduma ya uhakika ya maji kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Bw. Robert Sunday ameongoza majadiliano kuhusu uendelezaji wa rasilimali za maji nchini.
Majadiliano hayo yamefanyika Mtumba, jijini Dodoma.
Mjadala huo utakaodumu kwa siku tatu umewakutanisha wadau wa Sekta ya Maji wakiwamo washirika wa maendeleo na kutoka sekta ya umma.
Miongoni mwa mambo muhimu katika kikao hicho ni namna yakusimamia na kufuatilia fedha zinazo tolewa kwajili ya shughuli za usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji na ubora wa maji nchini.