Maafisa Habari kutoka Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakifuatilia mada kuhusu Mchango wa TARURA katika Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwenye Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara, iliyowasilishwa na Mratibu wa Miradi ya Ufadhili wa Nchi za Ulaya (Agriconnect), Mhandisi Claver Mwinuka, katika Ukumbi wa Jiji Mtumba, jijini Dodoma.
Lengo la mada ni kuwajengea uelewa Maafisa Habari wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu mchango wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya miundombinu ya barabara, sambamba na mafanikio yaliyopatikana chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, ili kuwawezesha kutoa taarifa sahihi na zenye kuelimisha kwa umma.