Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Paul Deogratius aliyemwakilisha Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan mitawi, akizungumza wakati wa Kikao kazi cha Mapitio ya Rasimu ya Dira ya Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto iliyofanyika leo Mei 23, 2025 jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko ya Tabianchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Salim Hamad Bakari akizungumza wakati wa Kikao kazi cha Mapitio ya Rasimu ya Dira ya Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto iliyofanyika leo Mei 23, 2025 jijini Dodoma.
Washiriki wakiwa katika Kikao kazi cha Mapitio ya Rasimu ya Dira ya Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto iliyofanyika leo Mei 23, 2025 jijini Dodoma.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kikao kazi cha Mapitio ya Rasimu ya Dira ya Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto iliyofanyika leo Mei 23, 2025 jijini Dodoma.
………………
Serikali imesema zinahitajika hatua madhubuti na za kimkakati katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zinakadiriwa tabianchi kugharimu hadi asilimia tatu ya Pato la Taifa kwa mwaka.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Paul Deogratius aliyemwakilisha Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan mitawi, wakati wa Kikao kazi cha Mapitio ya Rasimu ya Dira ya Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto iliyofanyika leo Mei 23, 2025 jijini Dodoma.
Dkt. Deogratius amesema kukamilika kwa mkakati huo kutanufaika na maandalizi ya Dira ya Taifa 2050 ambayo moja ya nguzo tatu za utekelezaji wake ni Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, hivyo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa malengo ya muda mrefu ya Dira ya Taifa 2050 yanawekewa msingi imara wa kuyafikia.
“Mathalani, hali ya hewa ya Dodoma imebadilika katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kipindi hiki kilipaswa kuwa cha masika tofauti na hali tunayoshuhudia. Mabadiliko ya tabianchi yanaathiri sekta zote za kiuchumi na kijamii,” alisema.
Ameongeza kuwa Rasimu ya Dira ya Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto inalenga kutoa mwelekeo wa hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kufanikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii sambamba na kupunguza uzalishaji wa gesi joto na kuimarisha uhimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Vilevile, amesema Rasimu ya Dira imezingatia vipaumbele vya taifa na kuweka msingi wa mabadiliko ya kiuchumi, usawa wa kijamii, pamoja na kuvutia uwekezaji kupitia sera na mazingira wezeshi.
Dkt. Deogratius ametoa shukrani kwa Serikali ya Ujerumani kupitia Asasi ya 2050 Pathways Platform kwa ushirikiano katika maandalizi ya Dira ya Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko ya Tabianchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Salim Hamad Bakari alisema ushirikiano na Ofisi ya Makamu wa Rais utaleta tija katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kwakuwa Zanzibar ni eneo la kisiwa limekuwa likikabiliwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabianchi hususan kuongezeka kwa kina cha bahari na kusabakatika mafuriko kwenye maeneo ya fukwe.
Naye Bi. Rose Mbezi kutoka Wizara ya Kilimo alisema baadhi ya shughuli za kilimo zinaathiriwa na uzalishaji wa gesi joto hivyo kikao kazi hicho kinawezesha kutoa mwelekeo katika kuonanisha sera na vipaumbele katika kutekeleza dira.