Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mheshimiwa Baraka Luvanda walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kansai ulipo Osaka nchini Japan ambako atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maonesho ya World Expo 2025 Osaka.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan. Vilevile Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970). (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kansai ulipo Osaka nchini Japani ambako Waziri Mkuu atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hssan kwenye Maonesho ya World Expo 2025 Osaka. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan. Vilevile Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho hayo ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970). (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioambatana nae katika safari ya Japan ambako atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hssan kwenye Maonesho ya World Expo 2025 Osaka, wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shariff Ali Shariff na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Zanzibar, Ali Suleiman Ameir.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.Vilevile Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970). (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)