Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ivory Coast mwenye Makazi nchini Nigeria Mhe. Balozi Selestine Kakele mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Félix Houphouët Boigny uliopo Jijini Abijan nchini Ivory Coast leo tarehe 24 Mei 2025. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mikutano ya Mwaka ya Bodi za Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itakayofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 30 Mei, 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Félix Houphouët Boigny uliopo Jijini Abijan nchini Ivory Coast leo tarehe 24 Mei 2025. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mikutano ya Mwaka ya Bodi za Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itakayofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 30 Mei, 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Elimu wa Ivory Coast Mhe. Marietou Kone wakati akiwasilikatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Félix Houphouët Boigny uliopo Jijini Abijan nchini Ivory Coast leo tarehe 24 Mei 2025. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mikutano ya Mwaka ya Bodi za Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itakayofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 30 Mei, 2025.