UVCCM YAZINDUA KAMPENI YA MATEMBEZI KIJANI FIRST TIME VOTERS
Na.Alex Sonna-DODOMA
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umezindua kampeni ya matembezi Kijani First Time Voters yenye lengo la kuhakikisha Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaibuka na ushindi katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Matembezi hayo yalianza katika uwanja wa Jamhuri na kupita maeneo mbalimbali na Kisha kumalizikia katika uwanja wa Mtekelezo Jijini hapa na kupokelewa na Mwenyekiti wa VCCM Taifa,Mohammed Kawaida.
Matembezi hayo yaliongozwa na Wenyeviti wa Mikoa ya Tanzania pamoja na vijana kutoka Wilaya za Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa,Kawaida amesema lengo la matembezi hayo ni kuhakikisha CCM inazima zote na inawasha kijani katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
“Nataka tuwaambie rangi zitaongea leo hapa tumezima zote tumewasha kijani tunataka katika uchaguzi Mkuu kuhakikisha tunashinda kwa kishindo,nataka tuwaambie rangi zitaongea tunataka tupate ushindi mkubwa na wa kishindo,”amesema Kawaida.
Kwa upande wake,Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Rehema Sombi amesema vijana wana akidi kubwa hivyo ni lazima waunge mkono utekelezaji wa ilani kwa kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa.
“Tuendelee kuwakumbusha kijani ni ustawi,ninyi kuwa vijana wa CCM kwa kweli tuilinde amani na itakapofika Oktoba chaguo letu ni Samia Suluhu Hassan.
“Kijani itaendelea kuhuisha amani,tusiwe wakwanza kukwaza amani.Niwaambie vijana mawazo yote yanaendana na kijani sisi tushuke chini tukawaelekeze tukizungumza kijani inamaanisha nini,”amesema





