Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maonesho ya Kimataifa ya Osaka( World EXPO OSAKA 2025) nchini Japan, Mei 25, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World EXPO OSAKA 2025) nchini Japan wakimsikiliza Waziri Mkuu,Kassim Majliwa alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maonesho hayo, Mei 25, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaliamiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Fujii Hisayuki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World EXPO OSAKA 2025) nchini Japan, Mei 25, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaliamiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Fujii Hisayuki katika Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World EXPO OSAKA 2025) nchini Japan, Mei 25, 2025. Kulia ni Mkewe Mary Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaina na viongozi walioshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World EXPO OSAKA 2025) alipowasili kwenye maonesho hayo nchini Japan, Mei 25, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wasanii wa kikundi cha Dar Creators wakitumbuiza katika Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World EXPO OSAKA 2025) nchini Japan, Mei 25, 2025. Kulia ni Mkewe Mary Majaliwa. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maonesho hayo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na mkewe Mary wakitanzama burudani iliyoporomoshwa na Kikundi cha Taarabu cha Rahat Zamani cha Zanzibar katika Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World EXPO OSAKA 2025) nchini Japan, Mei 25, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha ya tingatinga, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Fujii Hisayuki (wa pili kulia) katika Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World EXPO OSAKA 2025) nchini Japan, Mei 25, 2025. Kulia kwake ni Mkewe Mary Majaliwa na kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizungumza na Dkt. Kizusue Konoike katika Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World EXPO OSAKA 2025) nchini Japan, Mei 25, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ushirikiano wa Tanzania na Japan umezidi kukua katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia umezidi kuimarika siku hadi siku, ambapo mauzo ya biashara kati ya nchi hizo yameongezeka kutoka dola za Marekani bilioni saba mwaka 2023 hadi bilioni 37 kwa mwaka 2024.
Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumapili, Mei 25, 2025) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World Expo Osaka 2025) yanayoendelea nchini Japan.
Amesema Wajapan wanapenda sana bidhaa kutoka Tanzania zikiwemo za kilimo kama chai, kahawa, ufuta, tumbaku, tingatinga, vinyago, katani, viungo kama karafuu pamoja na madini mbalimbali yanayopatikana nchini.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan na duniani kote waje kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya elimu, afya, miundombinu, nishati, kilimo, utalii kwani Tanzania imeweka mazingitra mazuri ya uwekezaji na pia ina amani na utulivu.
“…Tanzania licha ya kuwa na fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo ardhi yenye rutuba, amani na mazingira tulivu, pia ni kitovu cha biashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Kusini na Kati kwa kuwa inapakana na nchi saba ambazo ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Zambia, Malawi na Msumbuji hivyo kuwawezesha wawekezaji kupata masoko ya uhakika katika mataifa hayo.”
Waziri Mkuu amesema Serikali ipo katika mchakato wa kuvifanyia maboresho viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu sabasaba ili viwe na hadhi ya kimataifa na kuwezesha kufanyika mikutano na maonesho ya biashara ya kikanda na kimataifa.
Monesho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanziba wakiwemo Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi mbalimbali.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho hayo ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).
Kesho (Jumatatu, Mei 26, 2026), Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kushiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan. Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili na viongozi wa Serikali ya Japan, mashirika ya maendeleo na watendaji wakuu wa makampuni mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan. (mwisho)