WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 03, 2025 ni mgeni rasmi katika jukwaa la vijana na mazingira linalofanyika katika ukumbi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Jukwaa hilo la vijana na mazingira lina malengo ya kuwaunganisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini, kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya mazingira pamoja na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kubuni na kutekeleza mikakati ya kutatua changamoto za mazingira nchini.
Tuliko hili ambalo ni sehemu ya maadhimisho kuelekea siku ya Mazingira Duniani, limeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa kushirikiana na Taasisi ya Africa Carbon Agency.