Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri na Mazingira na Hali ya Hewa wa Sweden Mhe. Romina Pourmokhtari kando ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari unaofanyika Jijini Nice nchini Ufaransa leo tarehe 10 Juni 2025.
Mazungumzo hayo yamelenga kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Sweden katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kubadilishana maarifa katika kilimo janja, kuhamisha teknolojia za kisasa za kulinda mazingira pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia.