Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, tarehe 10 Juni 2025 imekutana na kufanya kikao na Wakuu wa Vitengo vya Sheria wa Halmashauri za Mkoa wa Mwanza.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mjini Mwanza na kimeongozwa na Wakili wa Serikali wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Kadyemela Lushagara
Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kukutana na Wakuu wa Vitengo vya Sheria Mkoa wa Mwanza na kuwafahamisha juu ya uwepo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mkoa wa Mwanza na huduma za kisheria zitolewazo na Ofisi hiyo.
Kikao hicho pia kimejadili na kuazimia namna bora ya Mawakili wa Serikali wa Halmashauri kutekeleza majukumu yao katika mwaka wa fedha ujao 2025/2026 hasa katika eneo la Uingiaji wa Mikataba, Usimamizi wa Miradi ya Uwekezaji na Maendeleo, Uendeshaji wa Kamati za Ushauri wa Kisheria za Wilaya, na
Ushiriki wao katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2025.