Meneja wa hotel hiyo ya kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge , Beatrice Dimitris Dallaris akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
………….
Happy Lazaro ,Arusha .
HOTEL ya kitalii ya nyota tano ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha imerudi kwa kasi huku ikijipanga katika kutoa huduma zilizo bora zaidi kwa wageni wake sambamba na kuboresha miundombinu mbalimbali kwa lengo la kutangaza sekta ya utalii .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye kilele cha maonesho ya utalii ya Karibu -Killifair ,Meneja wa hotel hiyo ya kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge , Beatrice Dimitris Dallaris ambaye amekuwa miongoni kwenye kilele hicho amesema kuwa, sekta ya utalii nchini inazidi kukua kwa kasi sana na hii imetokana baada ya Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuifungua nchi kupitia filamu ya The Royal Tour ambayo imeleta mafanikio makubwa sana kwenye sekta hiyo baada ya mpito wa CORONA.
“Nimefurahi sana kuona maonesho haya yameendelea kutanuka na kuwa makubwa sana kwani ata nchi nyingi za majirani zimeshiriki na watu mbalimbali wakionyesha bidhaa zaina zote zinazo tumika kwenye sekta hii ya utalii .”amesema Beatrice.
“Nimepewa nafasi ya kipekee kuja hapa nikimwakilisha mkurugenzi mkuu wa Ngurdoto Mountain Lodge ‘Joan Auye Mrema na sisi kama Ngurdoto Mountain Lodge tunaangukia katika muhimili wa sekta hii ya utalii ambao kwa sasa imeleta sura mpya na mabadiliko makubwa sana na kuwa gumzo kila kona ya dunia.”amesema .
“Sisi kama Ngurdoto Mountain Lodge tunapenda kunatoa shukrani za kipekee kwa Rais wetu, Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ameweza kutupia jicho la pili kwenye sekta ya utalii na sasa tumeamka na kuanza tunafanya vizuri, kwa pamoja tutaendelea kuunga juhudi zake katika kukuza na kuendeleza utalii kwa kuhakikisha sekta ya utalii haipoi inasonga mbele na kuendelea kuvutia wenyeji, majirani na watalii zaidi .”amesema .
Beatrice aneongeza kwa kusema kuwa,lengo la kuu la kutembelea maonesho hayo ni kuweza kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na huduma nyingine nyingi na kupata fursa ya kuitangaza upya hotel hiyo kwa wananchi pamoja na wadau wa utalii ndani na nje ya nchi watambue kuwa Ngurdoto Mountain Lodge bado ni hotel ya kitalii na bado inashikilia nyota zake tano na wapo kivingine zaidi.
“Hivi karibuni wameweza kupata baraka ya kuweza kuhudumia Gala Dinner ya TAA-ACI AFRICA 2025, sio ivyo tu walipata nafasi ya kipekee ya kuhudumia mkutano mkubwa wa chama cha waendesha Ofisi za Serikali TAPSEA uliokuwa na washiriki zaidi ya elfu tano ambapo baadhi yao waliweza pia kuhudumiwa ya malazi, na kupata huduma ya usafiri kutoka wiwanja vya ndege na kuweza kutembelea vivutio mbalimbali kupitia kampuni yao ya utalii.
Ameongeza kuwa ,kama mdau wa utalii anaipenda sana sekta hiyo kwani ambayo ameifanyia kazi kwa zaidi ya miaka 18 sasa na amepata uzoefu ndani ya sekta hiyo kiujumla, aneongeza kwa kusema bado hajachoka kujifunza.
Aidha ameiomba serikali kuendelea kuwaangalia na kuwasaidia katika kuhakikisha sekta hiyo inazidi kupaa zaidi ili watu kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo na zijazo kwenye nchi yetu.
“Nawakaribisha watanzania wote kwa ujumla, nchi za majirani na dunia kwa ujumla kwani Ngurdoto Mountain Lodge ipo na ina bei za kawaida sana kuanzia malazi ya vyumba aina mbali mbali venye uwezo wa kulaza watu 394 kwa mara moja na miongoni ni presidential villa ambazo zipo 15 na pia kuna vivutio vingi kama viwanja vya michezo mbalimbali , bwawa la kuogelea kwa wakubwa na watoto, michezo ya watoto na sehemu ya mazoezi.”
Aidha amewataka wadau kuutumia ukumbi wao wa kimataifa kwa shughuli zao mbali mbali kwani ukumbi wao una uwezo wa kuchukua watu wengi kufikia elfu nane wakiwa wamekaa wote na ndani ya ukumbi na sehemu ya kula chakula wakiwa wamekaa kwa kiwango hicho hicho.”amesema.
Ameongeza kuwa ,wana kumbi zingine ambazo zinaweza kuchukua watu mia tano, mia nne , na nyingine ambazo zina uwezo wa kuchukua watu mia moja na nyingine ndogondogo.
“Tunashukuru sana kwamba watu wameendelea kutuunga mkono na kutufanya hoteli yetu ya Ngurdoto Mountain Lodge kuendelea kusonga mbele na inatuwezesha na sisi kuendelea kuunga mkono na kwa pamoja tuzidi kukuza sekta yetu ya utalii ili izidi kuwa bora zaidi na kupaa zaidi na zaidi .”amesema .
Ameongeza kuwa, kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro hadi kufika hotel ya Ngurdoto Mountain ni kilometa 27 tu na kutoka Arusha Mjini pia ni kilometa hizo hizo 27, ambapo kutoka hotelini hapo hadi hifadhi ya Arusha ni kilometa 7.5 .