Serikali itaendelea la kutoa mafunzo ya Mtaala uliboreshwa kwa walimu wote nchini ili kuhakikisha wanakuwa bora katika eneo la ufundishaji na ujifunzaji shuleni huku akiwataka walimu wote waliopata mafunzo ya somo la elimu ya biashara nchi nzima kuwa na mtizamo mpya katika kufundisha somo hilo .
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Elimu kutoka ofisi ya Rais na Utawala Bora TAMISEMI, Bw. Atupele Mwambene aliyemwakilisha mgeni rasmi , Katibu TAMISEMI ,Bw. Adolf Nduguru kwenye ufungaji wa mafunzo ya walimu wa ajira mpya wa somo la Elimu ya Biashara katika mtaala ulioboreshwa leo tarehe 11/6/2025 katika chuo cha Ualimu Korogwe , Mkoani Tanga.
Amewataka kuhakikisha wanakuwa na mtizamo chanya katika kufundisha somo hilo la elim u ya baishara kwa kuhakimisha wanakwenda shuleni kuwafundisha walimu vyema ili waweze baadae kutumia somo hilo katika kujiajiri wenyewe kwa namna watakavyoweza kuwandaa .
“Hakikisheni mnakuwa na mtizamo chanya mnaporejea katika vituo vyenu vya kazi haya mafunzo yakalete mabadiliko kwa wanafunzi nchini kwani maboresho kayika mtaala umewekwa masuala ambayo yatamsaidia mwanfunzi katika kujifunza vyema suala la biashara” amesema Bw. Mwambene.
Pia ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha elimu nchini ikiwemo kutoa ajira kwa walimu nchini pamoja na kuidhinisha fedha za mafunzo kwa walimu wote nchini na kuendelea kuimarisha sekta ya elimu.
Katika hatua nyingine ameitaka Tassis ya Elimu Tanzania (TET)kuhakikisha inaendelea kuimarisha mafunzo endelevu kazini(MEWAKA) kwa walimu wote ili waweze kuendelea kujifunza katika jumuia za ujifunzaji kuongeza ujuzi na uelewa wa masomo kazini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba amewaasa walimu hao kuwa chanzo cha mabadiliko katika ufundishaji wao kwa somo hilo la elimu ya biashara na kusema kuwa mbinu walizojengewa katika mafunzo hayo wazitumie vyema katika kuhakikisha wanakuwa bora.
“Hakikisheni mnazingatia yote mliyofundishwa kwenye mafunzo haya myatumie vyema mnaporejea katika viruo vyenu vya kazi , naomba sana mzingatie yote mliyofundishwa ili mkalete mabadiliko”amesema, Dkt. Komba
Naye Afisa Elimu wa Korogwe Bi.Mary Mmari amesema kuwa mafunoz haya yanatija kwa walimu wote walioweza kuyapata hivyo amewaomba walimu hao wawe sehemu ya mabadiliko.
Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserekali la EDUCATE, Bw. Nelson Musikula amesema, kama wadau wataendelea kutoa ushrikiano katika kuinua elimu nchini hasa katika somo la elimu ya biashara ili kuwezesha wanafunzi wote nchini wanapata uelewa na kuweza kujifunza namna ya kuanzisha biashara.
Jumla ya walimu idadi ya 1913 wamepata mafunzo ambapo katika kituo cha chuo cha ualimu Tabora jumla ya walimu walikuwa 513, kituo cha chuo cha Morogoro ni idadi ya 791 huku Chuo cha Ualimu Korogwe wakiwa idadi ya 609.