Na Sophia Kingimali, Dar es salaam.
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tuzo za 32 za kimataifa za utalii kwa kanda wa Afrika na bahari ya hindi ambapo wageni zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki.
Pia,wadau wa sekta ya utalii katika mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuchangamkia fursa za mkutano huo katika kuwahudumia wageni hao.
Akizungumzia mkutano huo leo june 11,jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya utalii (TTB) Ephraim Mafuru amesema lengo la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa wadau wa utalii Duniani.
“Uwepo wa tuzo hizi nchini ni jitihada za Rais Dk Samia Suluhu hassan tunapaswa tumpongeze Tuzo kama hizi ziliwahi kufanyika miaka ya nyuma ambapo hazikuwa kwa ukubwa kama ilivyo sasa”,amesema Mafuru.
Amesema kuchaguliwa kwa Tanzania kuwe mwenyeji wa Tuzo hizo kwa nchi za Afrika pia kumetokana na ushindi wanchi katika tuzo zilizopita kwani iliongoza kwa kuwa na tuzo 5 tofauti na nchi nyingine za Afrika.
“Shughuli kama hii mwaka jana 2024 ilifanyika Mombasa kenya Tanzania ili shinda tuzo tano ambapo bodi bora ya utalii ya utalii Afrika ilichukua TTB,kivutio bora cha utalii Afrika ilikuwa mlima Kilimanjaro, hifadhi ya taifa bora Afrika ilikuwa Serengeti, kivutio bora cha safari Duniani sasa mafanikio haya hayaji tu hivi hivi ni kazi kubwa imefanyika ikiongozwa na Rais wetu”,Amesema.
Aidha amwongeza kuwa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na utalii zitashiriki ambapo washiriki 38 kutoka sekta bifasi na 12 kutoka Serikalini watashiriki.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli ya Johari Rotana ambae ndio ‘Host’ wa tuzo hizo Ahmed Said amesema wao kama hoteli wamejipanga vyema kuhakikisha wanawahudumia vyema wageni wote watakaofika kwenye tuzo hizo.
Naye,Mkurugenzi wa Masoko kutoka hospitali ya Shifaa Victoria Tarimo amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanatoa huduma za kimataifa katika kuwahudumia wageni hao ambao watapata changamoto za kiafya wakati wa tuzo hizo.
“Sisi tumejipanga vizuri na tunavifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya kuwahudumia na tutakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha tunawapa huduma nzuri kwani tunavifaa vya kisasa na wataalam wa kutosha lakini pia tutakuwa na gari la wagonjwa kwa ajili ya dharura”,amesema.
Amesema Hospitali imejipanga kusapoti agenda ya Rais Dk Samia ya Tiba utalii kwa vitendo.
Tuzo hizo zilianIshwa mwaka 1993 lengo likiwa kutambua mchango wa wadau walipo katika sekta ya utalii katika maeneo mbalimbali Duniani ambapo sasa zinatarajiwa kufanyika june 26,2025 katika hotel ya Johari rotana jijini Dar es salaam ambapo hoteli hiyo pamoja na hospitali ya shifaa ndio watakaohudumia watu katika Tuzo hizo.