Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mwanza
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Stephen Wasira amewasili mkoani Mwanza na kisha ataelekea mkoani Geita kwa ajili ya kuanza ziara ya siku tatu katika mkoa huo.
Wasira amewasili leo Juni 15 mwaka 2025 katika Uwanja wa Ndege Mwanza ambapo amepokelewa na viongozi wa Mkoa huo kisha amepata nafasi ya kumsalimia na kufamfariji Mama Getrude Mongella ambaye hivi karibuni ameondokewa na mumewe mzee Silvin Ibengwe Mongella aliyezikwa Mwanza.
Hata hivyo kesho Juni 16 mwaka huu Wasira ataanza ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Geita ambapo atakutana na wana CCM na pia kushiriki vikao vya ndani ya Chama ngazi ya Wilaya na Mkoa vitakavyohusisha pia viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Mbali ya kuwa na ziara katika Mkoa wa Geita ,Makamu Mwenyekiti Wasira pia anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa daraja jipya la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Pia uzinduzi wa daraja hilo ambalo limejengwa katika Ziwa Victoria unatarajiwa na kushuhudiwa pia na viongozi mbalimbali pamoja na maelfu ya wananchi wa Mwanza na mikoa jirani.