

Na Mwandishi Wetu, MwanzaMAKAMU Mwwnyekiti wa Chama Cha Mqpinduzi (CCM) Stephen Wasira amesema uchaguzi ukuu sio ajali hivyo wabunge na madiwani wote wanajua kwamba kila baada ya miaka mitano kuna uchaguzi hivyo wale waliokuwa wanajifungia vioo kwenye
magari wajue wakati umefika.
Pia amesema katika uchaguzi mkuu ni vema pia wanaotaka kugombea wakapima uwezo wao kama ambavyo unavyotaka kupima kina cha maji lazima utumie fimbo kujua nguvu ya maji kabla ya kuvuka ili usisombwe na maji.
Akizungumza na viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Wasira alitumia nafasi hiyo kuwataka wana CCM kujiandaa kwenda kutiki ifikapo Oktoba na kwa nafasi ya urais tayari wamepitisha jina la Dk.Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dk.Emanuel Nchimbi.
“Kwa upande wa urais tumemaliza tumeshaweka mgombea wetu Dk.Samia Suluhu Hassan na kazi yetu ni kumuuza kwa wananchama na wananchi .Kwa wabunge kama ubunge unaisha Juni 27 ndio maana hauwapi presha maana tangu walipoingia maana walijua ikifika miaka mitano uchaguzi unafanyika.
“Kwa hiyo uchaguzi sio ajali… kama wewe unauogopa labda hukufanya maandalizi maana wako watu katika jamii hata wale waliowachagua hawawajui wale ndio wenye kupata presha… sasa kama unafunga vioo unawapita watu usilaumu watu,”alisema Wasira.
Akieleza zaidi Wasira alisema amekuwa mbunge kwa miaka 30, hivyo analijua bunge vizuri na kueleza kwamba ubunge unavyopatikana unapatikana kwa kujenga uhusiano na watu, ukijenga uhusiano na watu mambo yako yanakuwa rahisi
“Kazi yangu si kumpigia mtu debe mbunge ila ukifika kwa wana wana CCM na lakini ukifika hapa kwa mfano unasikia kaulimbiu za wananchi au wana CCM wanamtaja wanayemtaka.Kwa wabunge ambao walifanya kazi zao vizuri wala hawana wasiwasi.”
Akizungumza zaidi Waira alisema Pia Wasira alisema uchaguzi umefika na wanachama wana haki ya kuchukua fomu ila alishauri kwa wale wanachama wapya wanaotaka ubunge wakapima nguvu ya waliopo au waliomaliza muda wao.
“Wakati sisi zamani tukiwa watoto ukitaka kuvuka mto maana madaraja hayakuwepo na mito kama inatiririka hivi unaenda na fimbo, unatanguliza fimbo uone kama fimbo itatikiswa na maji, ikitikiswa na maji mpaka take kwenda huingii pale maana utaenda wewe,
“Nataka wenzangu niwaambie wanaotaka ubunge hakuna mtu anawazuia hata kidogo, ushauri wangu watembee na fimbo kwanza wapime kina cha maji wakiona kina ni kigumu wasubiri hadi mto upungue sasa sijui kama utapungua kabla uchaguzi, huo ni ushauri,”alisema Wasira.
Kuhusu utaratibu wa kupata wagombea aliwakumbusha kuwa Chama hicho wameongeza idadi ya wajumbe ambao watapiga kura kupendekeza wagombea ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu.
“Sasa niwaambie kwa nini tumeongeza wapigakura za maoni maana zamani walikuwa wachache sana, sasa wachache wale mtu alikuwa anaweza kutaka nafasi lakini ana pesa anauliza wako wangapi (kwa awali Magu walikuwa 940, lakini sasa ni zaidi ya 10,000)…
“Kama unahela za kuhonga watu wote hao si ununue nyavu uvue samaki maana bungeni huwezi kupata milioni 700 wanawadanganya tu kwamba wabunge wana hela nyingi. Wanapata fedha kwa kufanya shughuli zao, lakini wabunge ambao hawana shughuli wanapewa pesa kwa ajili ya kununua gari na matengenezo kwa kila muda.
“Na mshahara wao ni wa kawaida hawana tofauti na wa Nasari (Mkuu wa Wilaya ya Magu, Joshua Nasari), nyingine hizi ni hela za vifaa, mafuta maana gari moja ya tabia zake ni uitengeneze.Kwa hiyo ukiona wabunge wanakwepa kwenda kwa watu ni hela ile haiwatoshi kwa hiyo wanataka wabakishe chenji,”alisema Wasira.
Alifafanua kama wewe(mgombea ubunge) una bilioni moja ni vema uende uvue samaki, ufanye, ufanye vizimba au uwekeze katika kununua mazao utapata faida zaidi kuliko kwenda Bunge maana utaokosa na utachanganyikiwa bilioni imeenda na ukiulizwa umeipeleka wapi utasema sijui na uliowapa hawakurudishii maana wale hawana huruma.
“Kwa hiyo tukasema tuweke watu wengi tunataka wapiga kura wa maoni mnapopiga kura mzingatie sauti ya wananchi, zingatieni sauti ya wananchi.CCM hatuchagui mbunge ila tunampendekeza tu anaenda kwa wananchi kwa ajili ya kumchagua.
“Hivyo sikilizeni wananchi wanasemaje kama wanasema mgombea anatosha basi tupige kura kwa kuzingatia maoni ya wananchi ili kazi yetu kwa wananchi isiwe ngumu kama kusukuma mawe, iwe rahisi kwa sababu mmetuletea mgombea anayekubalika kwa wananchi kabla ya saa mbili tunakuwa tumeshatangaza matokeo.”