Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mfumo wa e-Wekeza utakaomuwezesha Mtumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida, alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Wiki ya Utumishi Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Juni 23, 2025. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)