Na. Vero Ignatus Arusha
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi – PDPC, Bw. Emmanuel Mkilia amezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha kuwa Taarifa binafsi zinalindwa sambamba na haki za binadamu zipewe kipaumbele.
Mkilia ameyasema hayo leo Juni 23,2025 Jijini Arusha wakati akifunga mafunzo ya maafisa wa Taasisi za Umma yaliyoandaliwa Tume hiyo kushirikiana na Taasisi Usimamizi wa vihatarishi Tanzania (IRMT) kwa kuwataka washiriki hao wa mafunzo hayo ya siku tatu waweza kupata mbinu mbalimbaki na maarifa mapya katika ulinzi wa taarifa binafsi, kutambua vihatarishi kabla havijatokea
Ili kulinda Taarifa binafsi za wateja wenu kunahitajika mbinu za kiutendaji na kimkakati, tubawahimiza wasimamizi wa vihatarishi , kufanya tathmini za Mara kwa mara, kuanzisha na kusimamia Sera za ulinzi wataarifa, binafsi, kuweks katijs tehama salama na kuhakikisha mfumo ya kieletroniki inalindwa kwa teknolijiaya kisasa, kutoa magunzo wa tymidhi
Mkilia amesema Mafunzo hayo kwa sasa kwa kwani kumekuwepo kwa changamoto za kulindwa kwa faragha wakati wa utekelezaji wa Majukumu hivyo kila Taasisi inapaswa kulindwa Taarifa zake binafsi kwa usahihi kwa kuwa makini wanatumia telnolojia ya habari na mawasilino kwani inakwenda kwa kasi
“Hakikisheni Taarifa binafsi zinalindwa sambamba na haki za binadamu, changamoto zimekuwepo teknolojia z inakwenda kwa kasi tunasema hayo kwasababu tunawekeza nguvu Pamela na fedha hivyo ni vyema kutambua viatarishi kabla havijatokea japokuwa wapo watumishi ambao siyo waaminifu ambao wanavijisha taarifa. Alisema
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Chuo cha Usimamizi wa Vihatarishi (IRMT) Bw. Christopher Njovu ametoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kuzingatia kupata elimu hiyo na kuhakikisha maafisa wao wanakuwa wataalamu walioidhinishwa kusimamia vihatarishi.
“IRMT tunatoa mafunzo ya kutengeneza na kuthibitisha wataalamu wa usimamizi wa vihatarishi nchini Tanzania, hivyo nawasihi mje mpate mafunzo haya na vyeti vya kuwathibitisha kuwa ni wataalam wa eneo hili, kufanya tafiki ya masuala halisi ya vihatarishi na kuandika ripoti ya fedha. Alisema
Mafunzo hayo ya siku tatu kuanzia leo tarehe 23 Juni 2025 ni moja ya njia ya kuhakikisha taasisi za umma na binafsi zinakuwa na utaratibu wa kutambua viashiria vya vihatarishi hivyo na kuchukua hatua stahiki kabla hatari haijatokea
“Kumbukeni kwamba ulinzi wa taarifa ni jukumu la kila mmoja wetu na ni sehemu muhimu ya ujenzi wa imani na uaminifu kwa wateja wetu” Alisema
Aidha amewatakia kila la kheri katika madunzo yaliyomo mbele yenu ya kulinda taarifa binafsi na ninatarajia kuona mchango wenu chanya katika kuhakikisha kuwa taasisi zetu za kifedha na za watoa huduma ya mawasiliano ya simu zinakuwa salama na za kuaminika kwa wateja wetu.”
Mafunzo hayo yamewashirikisha wasimamizi wa vihatarishi, wajumbe wa bodi, wakuu wa Idara Wakuu wa Tehama wakaguzi wa ndani na nje, aidha ni kwaajili ya kupunguza madhara ya vihatarishi katika ulinzi wa taarifa binafsi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi – PDPC, Bw. Emmanuel Mkilia