Treni ya kwanza ya mizigo ya SGR imeanza safari yake ya kwanza kati ya Dar Es Salaam na Dodoma.
Treni hiyo yenye jumla ya mabehewa 10 imebeba mizigo mbalimbali ya takribani Tani 700.
Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) iliahidi na sasa imetimiza ahadi ya kuanza huduma ya usafiri wa treni za mizigo katika reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) ikiweka historia katika Jumuia ya Afrika Mashariki kuwa na treni ya SGR ya umeme ikisafirisha abiria na mizigo . Treni hii ya mizigo inatembea inatembea kwa kasi ya kilomita 120 kwa saa kulinganisha na mwendo wa kilometa 160 kwa saa kwenye treni za abiria.